Adobe kuja na toleo la Photoshop bure kwa wote

Imeandikwa na Alexander Nkwabi
Photoshop Bure Kwa Wote
Kwa mujibu wa mtandao wa The Verge, kampuni ya Adobe kuja na toleo la Photoshop bure kwa wote. Toleo hili la Adobe Photoshop hivi karibuni litapatiakana bure kwa watumiaji wote kama toleo la mtandaoni la programu kamili ya kuhariri picha. Toleo hili la bure kwa sasa linajaribiwa nchini Canada, ambapo watumiaji wanaweza kufikia Photoshop kupitia anwani ya wavuti iwapo watakuwa wameingia kwenye akaunti ya bure ya Adobe.

Adobe kuja na toleo la Photoshop bure kwa wote

Toleo hili la mtandaoni ambalo limeondolewa vipengele vingi, litamuwezesha mtumiaji kupata ufikiaji wa huduma za msingi za Photoshop. Toleo hili ambalo lilizinduliwa mnamo Oktoba linakuja kama zana ya kurahisisha kufanya maboresho na uhariri mdogo mdogo wa picha.

Adobe Kuja Na Toleo La Photoshop Bure Kwa Wote

Adobe inadai toleo la wavuti la Photoshop linapatikana chini ya mfumo wa “Freemium” yaani itakuwa bure japo zana au vipengele vingine vitahitaji kulipia ili uweze kuvitumia. Hivi sasa, zana nyingi, brashi na huduma zingine za Photoshop zinapatikana bure. Hata hivyo, Adobe inapanga kuondoa baadhi ya vipengele ambavyo vitakuwa vya kipekee kwa wanachama wanaolipa. Walakini, zana za “kutosha” zitapatikana kwa uhuru kufanya kile Adobe inadai ni kazi za msingi za Photoshop.

Adobe haijatoa tarehe kamili ya lini toleo hili la mtandaoni litaanza kutumika, kwaiyo sisi ambao tuko nje ya Canada tukae kwa utulivu tukisubiri.

Acha Ujumbe