air samoa waanza kutoza nauli kwa kutumia uzito wa mtu

Imeandikwa na Hemedans Nassor
Air Samoa Waanza Kutoza Nauli Kwa Kutumia Uzito Wa Mtu

kikawaida tumezoea nauli huwa inatozwa kwa kila siti. haijalishi we ni mwembamba wala mnene haijalishi una kilo nyingi wala chache. lakini kampuni ya ndege ya samoa imetoa mpya kwa kuanza kutoza nauli kwa kutumia uzito. hii inamaanisha watu wanene na wenye kilo nyingi watalipa nauli kubwa kuliko wembamba na wenye kilo chache.

Samoa-Air-640_Large_Verge_Medium_Landscape

 

hebu tuangalie mchanganuo wao wa nauli upoje

kilo 45 kwa sh 75,000 kwa safari fupi

kilo 45 kwa sh 300,000 kwa safari ndefu

 

hii ina maana kama una kilo 90 badala ya kulipa 75,000 utalipa 150,000

 

reason kubwa ya kuweka hii aina ya bei ni sababu uzito mkubwa unatumia mafuta mengi zaidi kuliko uzito mdogo ndege inapopaa

 

je mnaonaje aina hii ya kutoza nauli ni sahihi?

Acha Ujumbe