Ni namna gani eSIM itabadilisha mfumo wa teknolojia kuwa bora zaidi

Mwandishi Diana Benedict

Apple, Samsung na Google imeanza mazungumzo kwa watoa huduma zamitandao kuhusu kupitisha kadi za umeme (electronic SIM) kwa ajili ya smartphone za baadae. Samsung ndiyo kampuni ya kwanza ilianza kutumia huduma ya GSMA kuwezesha e-SIM kwenye kifaa cha Samsung Galaxy Gear S2, na mwanzoni mwa mwezi wa tisa mwaka huu Apple nao imeangazia huduma hiyo na kuiwezesha katika baadhi ya vifaa vyake zikiwemo Apple Watch series 3 na iPad, Google mwanzoni mwa mwezi wa kumi nayo ikatoa kifaa chake Google Pixel 2 zenye kuwezeshews kutumia huduma hiyo ya e-SIM. Makala hii itaangazia Ni namna gani e-SIM itabadilisha mfumo wa teknolojia kuwa bora zaidi

2016 12 16 t mobile esim 1

eSIM ni nini?

Hata kama wewe siyo mtaalamu wa mambo ya teknolojia, kuna uwezekano angalau umesikia kadi ya Moduli ya Utambulisho wa Msajili (SIM) au jina tulilolizoea “laini”. Ni kadi ndogo zinazopachikwa kwenye simu yako ambazo zinakusaidia kuunganisha kwenye mtandao wa mtoa huduma wako wa simu za mkononi.

Sasa, kadi za SIM zilizopachikwa (eSIMs) ni sawa SIM card za kawaida ila hizi zinakuja zikiwa tayari zimepachikwa kwenye simu kidijitali. Chapisho hili litajibu maswali kama, tofauti ya kadi za kawaida na eSim, kwa nini unaweza kuzihitaji, vifaa gani vinavyo, na jinsi ya kuvitumia.

Mpaka sasa umeshaanza kupata japo mwanga nini maana ya e-SIM, Kama jibu ndiyo tuendelee sasa,

l2JhGyinjAo9T0nug

Kuna tofauti gani kati ya eSim na kadi ya SIM ya kawaida?

eSIM ni toleo la kidijitali la SIM kadi halisi-kutambua kifaa chako karibu ili kutoa muunganisho wa mtandao. Huduma hii utaunganishwa kupitia mtandao husika wa simu unaotumia kupitia programu maalumu iliyomo kwenye simu janja yako hii inamaanisha hutahitaji kununua sim card mpya kila unapobadili simu au mtandao. eSIM inapatikana kwenye baadhi ya simu janja, tableti, drone na hata kwenye magari.

Faida/Hasara za eSIM katika jamii yetu.

Tumeitazamia huduma hii kama tulivyoielezea hapo juu sasa tukiangalizia katika faida na hasara za huduma hii ya e-SIM,

Tumekuwa na matukio mengi sana kuhusu wizi wa simu za mikononi, kwa upande mwingine tunawza sema hii ni moja ya faida kwa haitamuwezesha aliyeiba kwenda kubadiri sim card na kuweka yakwake au kutoa sim card yako ukose mawasiliano, kwa maana hiyo basi itamlazimu kuizima simu hiyo, na pindi atakapohitaji kuitumia simu hiyo itamlazimu ku-swap mawasiliano na itamhitaji kwenda kwa mtoka huduma za mitandao na hapo itakuwa rahisi ,mtu huyo kuwekwa mikononi mwa sheria.

Faida ingine ni uwezo wa kuweka hadi namba tano kwenye simu moja na kutumia namba mbili kwa wakati mmoja, hii itapunguza usumbufu wa kubaili laini kila mara unapotaka kutumia mtandao husika.

Changamoto kubwa ni usalama wa taarifa zako, kama simu au mtandao husika ukidukuliwa basi taarifa kuhusu wewe na simu yako zinaweza kuchukuliwa.

Je kwa Sasa eSIM inatumika kwenye simu zipi ?

Kwa sasa huduma ya eSIM inapatika kwenye baadhi ya vifaa vya kisasa ikiwemo simu janja, tableti, drones na hata magari. Pia kwenye vifaa vingine kama router na kadhalika.

Je Huduma ya eSIM Ipo Tanzania ?

Kampuni ya Zantel hapa Tanzania ndiyo iliweza kutumia huduma hiyo hasa katika vifaa vyake vya mtandao wa data USB – Modem kupitia mtoa huduma wake mkuu wa mtandao Etisalat, ila kwa upande wa simu za mkononi na vifaa vingine  huduma ya eSIM bado haijafika Tanzania, lakini kutokana na teknolojia hii kuendelea kutumika kwa wingi kwenye simu na vifaa mbalimbali tutarajie kusikia ujio teknolojia ya eSIM hivi karibuni.

 

Je umeipenda hii? tafadhari andika maoni yako hapo chini kwa kujaza email yako najina kamili!

Tufuatilie @MtaawaSaba ili usipitwe na matukio mbali mbali ya mitanadoni na ya kiteknolojia kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Google+ na Youtube, Pia usisite kutoa maoni yako kwa mhariri@mtaawasaba.com

Mwandishi Diana Benedict Mwandishi
Mitandao ya Kijamii
Diana Benedict. Digital Creator | IT Specialist | Graphics Designer | Web Designer | Web SEO | Contents Management | UI/UX Designer and Social Media Management.
3 Comments
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive