MtaawasabaMtaawasaba
  • Habari
  • Simu
  • Android
  • Kompyuta
  • Windows
  • Maujanja
  • StartUps
Mengineyo
  • Muongozo
  • Maujanja
  • Programu
  • Simu Janja
  • Teknolojia
Mtaawasaba
  • Kuhusu Sisi
  • Sera ya faragha
  • Vigezo na Masharti
  • Wasiliana Nasi
Mitandao
  • Facebook
  • Twitter
  • Instagram
  • YouTube
  • Newletters
© 2013 - 2023 Mtaawasaba Interactive
Unasoma Hizi ndizo sababu za Kampuni ya Facebook kubadili jina na kuitwa Meta
MtaawasabaMtaawasaba
  • Apple
  • kompyuta
  • Maujanja
  • Apps
  • StartUps
  • Magari
  • Mtaawasaba
    • Habari
    • Makala
    • Apps
    • Maujanja
    • Kompyuta
    • Simu Janja
    • Magari
    • Matukio
    • Muongozo wa mtumiaji
    • Mitandao ya kijamii
    • Programu
    • Teknolojia
    • Mfumo endeshi
    • Miwani Janja
    • Saa Janja
    • Televisheni
    • Utamaduni
  • Mengineyo
    • Microsoft
    • intaneti
    • Windows
    • SnapChat
    • TTCL
    • Tigo Tanzania
    • vifurushi visivyo rasmi
    • Google
    • halotel
    • Instagram
    • iOS
  • Kuhusu Mtaawasaba
    • Kuhusu Sisi
    • Sera ya faragha
    • Vigezo na Masharti
    • Wasiliana Nasi
Una akaunti? Ingia
Tufuate mtandaoni
© 2022 Mtaawasaba Interactive. Haki zote zimehifadhiwa.
Mtaawasaba > Featured > Hizi ndizo sababu za Kampuni ya Facebook kubadili jina na kuitwa Meta

Hizi ndizo sababu za Kampuni ya Facebook kubadili jina na kuitwa Meta

Imeandikwa na Alice Kimathi Mwaka 1 uliopita
Sambaza
Facebook kubadili jina na kuitwa Meta
Siku kadhaa zilizopita mtandao wa the Verge ulichapisha taarifa ya kwamba Kampuni Ya Facebook Mbioni Kubadili Jina. Taarifa ya Facebook kubadili jina na kuitwa Meta imekuja leo kupitia kwa mkurugenzi mtendaji wa Facebook, Mark Zuckerberg ambapo amesema Facebook inabadili ili kujitofautisha na mtandao wa kijamii wa Facebook kwani kampuni iyo kwa sasa inajihusisha na mambo mengine mengi tofauti zaidi ya mtandao wa kijamii huo.

kampuni yetu inahusishwa kwa karibu na bidhaa moja ambayo haiwakilishi kila kitu tunachofanya kwa sasa, na baadaye – mark Zuckerberg 

Akiongea kwenye mkutano wa ndani wa kampuni uitwao Connect, Zuckerberg ametangaza jina jipya la kampuni litakuwa Meta. Na Sasa kupitia utaratibu mpya, Facebook na mkusanyiko wa app na huduma zingine zitakuwa chini ya kampuni kubwa ya Meta, ambayo itakuwa chini ya Zuckerberg.

Unaweza Kusoma

Elon Musk ametangaza rasmi vita na Apple

Ramani, kutoka Tanzania yakusanya $32m kurahisisha mnyororo wa usambazaji

Teknolojia ya hali ya juu kutumika katika Kombe la Dunia la FIFA Qatar 2022

Tovuti ya iCloud ya Apple yapata muonekano mpya, inavutia zaidi.

Hizi ndizo sababu za Kampuni ya Facebook kubadili jina na kuitwa Meta

Taarifa ya Facebook kubadili jina na kuitwa Meta inakuja baada ya kampuni ya Facebook kukosolewa sana kutokana na kuvuja kwa “taarifa za ndani”  kuvujishwa na mtumishi wa zamani wa Facebook. Nyaraka hizo zina taarifa zinazoonesha jinsi taarifa za watu mashuhuri kutenganishwa na watu wengine, pia zikionesha jinsi kampuni ilivoshindwa kusimamia na kuzuia vikundi vyenye misimamo mikali kutumia mtandao wa Facebook kwenye uchaguzi wa marekani mwaka 2020, pia utafiti unaoonesha jinsi Facebook inavoahatarisha afya za vijana.

Facebook kubadili jina na kuitwa Meta kutaathiri kampuni tu, na sio mtandao wa kijamii wa Facebook, Instagram, Whatsapp na huduma zingine zote zitasalia na majina yao. Jina hili jipya litasaidia kuonesha uelekeo wa kampuni hii ambao ni “metaverse” – mazingira yanayoendeshwa na kompyuta ambapo watu wanaweza kuwasiliana kupitia teknolojia kama Artificial Intelligency (uelewa wa kutengenezwa) na Virtual Reality pamoja na teknolojia zingine za namna hiyo. Facebook imekuwa na wazo hili tangu iliponunua kampuni ya vifaa vya kuvaa kichwani vya virtual reality ya Oculus mwaka 2014.

Facebook sio kampuni ya kwanza kufanya mabadiliko ya jina kwa namna kama hii, mwaka 2015 Google walibadili mfumo wa kujiendesha na kuanzisha kampuni mama waliyoiita Alphabet. Ambapo Google ikabaki kuwa sehemu ya Alphabet, tofauti na Facebook ambayo inabadili kwa sababu tofauti na kuhakikisha inajitenga na jina la mtandao wake wa kijamii.

KWENYE Facebook, Meta
Sambaza chapisho hili
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Telegram Barua Pepe Nakili kiungo Durufu
Acha Ujumbe

Toa Jibu Ghairi kujibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Mtaawasaba Newsletter

Jiunge nasi kwa njia ya barua pepe tukujulishe kila inapotoka habari mpya

Zaidi Kutoka Mtaawasaba

Sasa unaweza pata Blue Tick kwa kulipia Instagram na Facebook

Sasa unaweza pata Blue Tick kwa kulipia Instagram na Facebook

Siku 4 zilizopita
Airtel yawa ya kwanza kuzindua huduma ya kadi za eSIM Tanzania

Airtel yawa ya kwanza kuzindua huduma ya kadi za eSIM Tanzania

Siku 5 zilizopita
Instagram yazindua Notes, Candid Stories, na Zaidi

Instagram yazindua Notes, Candid Stories, na Zaidi

Miezi 3 iliyopita
Umoja wa Ulaya waishinikiza Apple kuruhusu maduka mbadala ya programu kwenye iPhones na iPads

Umoja wa Ulaya waishinikiza Apple kuruhusu maduka mbadala ya programu kwenye iPhones na iPads

Miezi 3 iliyopita

© 2013 - 2023 Mtaawasaba Interactive. Crafted by Simba Creative

  • Kuhusu Sisi
  • Sera ya faragha
  • Vigezo na Masharti
  • Wasiliana Nasi
Go to mobile version
logo logo
Karibu Mtaawasaba!

Jaza taarifa kuingia Kwenye Akaunti Yako

Umesahau Nywila?