Fursa za Kazi

Mtaawasaba ni tovuti inayoandika kuhusu habari za teknolojia inayofikia maelfu ya wasomaji wanaotumia lugha ya kiswahili. Tunawapasha habari motomoto kadri zinavotufikia kupitia tovuti na njia zingine, pia tunatoa uchambuzi wa vifaa vya kielektroniki na teknolojia ili kuwasaidia watumiaji kufanya maamuzi sahihi ya chaguzi zao.

Lengo letu ni kupata timu ya vijana wenye vipaji na nia ya kuandika taarifa zenye ubora wa hali ya juu ili kuongeza idadi ya wasomaji wetu.

 

Kwa sasa tunahitaji waandishi wa kujitolea na wachangiaji katika upande wowote watakaochagua, habari, uchambuzi, makala au kipengele chochote ambacho watakuwa na amani kuandika.

Sifa za waombaji:

1.  Uzoefu wa kuandika habari za teknolojia, itapendeza zaidi kama utakuwa ulishaandika machapisho kadhaa.
2. Uwezo wa kuandika kwa kiswahili fasaha, na angalau kiingereza.
3. Uwezo mzuri wa kufafanua mambo.
4.  Hamu ya kutumia au kujaribu app mpya, software au teknolojia mpya
5. Mwenye kujua kinachoendelea kwenye dunia ya teknolojia
6. Awe na uwezo wa kutatua matatizo.

Eneo: Popote pale, sio lazima awe Dar es Salaam