Google yafanya Mabadiliko katika Matokeo ya kutafuta Picha

Imeandikwa na Kato Kumbi
Google Yafanya Mabadiliko Katika Matokeo Ya Kutafuta Picha

Kwa hoja ambayo bila shaka itasumbua watu wengi, Google imeondoa kifungu cha kutazama Picha katika utafutaji wa picha Google. Ikiwa utatembelea Google Images na ukihitaji kutafuta na kuchagua picha hautapata fursa ya kuona picha hiyo kwa ubora wake unaostahili kama ilivyokuwa mwanzo.

Google Yafanya Mabadiliko Katika Matokeo Ya Kutafuta PichaGoogle haijatoa maelezo ya moja kwa moja ya mabadiliko, ingawa mtu anaweza kudhani ni kuondoa huko ni moja ya Kitu ambacho wanataka google kujaribu kujipatia kipato. Kitufe cha ‘Angalia Picha’ kiliwapa roboti njia rahisi ya kuvuta picha kutoka kwenye mtandao wowote na kutumia kwa malengo yoyote ya kujinufaisha, na pia wakati watumiaji wanapopakua picha kwenye tovuti hawaoni matangazo yoyote ya tovuti au hata kupata fursa ya kushiriki na maudhui yaliyoizunguka picha hiyo.

Google Yafanya Mabadiliko Katika Matokeo Ya Kutafuta Picha

Habari hizi zimesambaa kutoka kwenye akaunti rasmi ya Google katika mtandao wa Twitter. Google iliwekea msisitizo kwamba sasa unapotafuta picha utahitaji kutembelea tovuti nzima kwa kunyakua picha nzima kwa matumizi yako mwenyewe.

 

Google Yafanya Mabadiliko Katika Matokeo Ya Kutafuta Picha

hata hivyo tayari kuna

Njia rahisi kurudisha kitufe cha view image kwenye matokeo ya google images

unaweza kurudisha kitufe cha view images kwa kutumia plugin hii hapa kama unatumia kisakuzi cha  Google Chrome na hii hapa kama unatumia mozilla firefox. 

kwa kuwa google wamefanya maboresho kwenye kisakuzi chao kipya cha Chrome chenye uwezo wa kuzuia matangazo, basi hatujui plugin hizi zitasalia kwa muda gani.

Tufuatilie kwenye mitandao mbali mbali ili usipitwe na Habari, Uchambuzi naMakala mbali mbali ya mitanadoni na ya kiteknolojia kwenye FacebookTwitterInstagram, Google+ na Youtube, Pia usisite kutoa maoni yako hapo chini au tuandikie barua pepe kwa [email protected]

Acha Ujumbe