Jinsi ya kuflash simu zote zenye MediaTek chipset

Mwandishi Alexander Nkwabi

Kama mwezi umepita nahangaika na TECNO ya mdogo wangu hapa nyumbani ambayo inajirestart kila muda mpaka betri iishe chaji, Nimehangaika nayo kwa mafundi lakini wote chali, Juzi nimeenda Kariakoo fundi akaniambia iyo lete 35k nikampa ikamshinda nikaenda kwa wawili watatu chali, sasa nikaamua kutake matter in my hands, jana nimefanikiwa kuiflash na kuiroot kabisa, nikaona si vibaya kushare ugunduzi wangu huu….

mediatek chip 25

Jinsi ya kuflash simu zenye MediaTek chipset

Simu za MTK kama zilivyo processor nyingine huwa na shida ya kustuck, autorestart, kutokuwaka kabisa na kuleta matangazo mengi kwenye screen (ads)

Nafikiri simu za Infinix, Dogee, Itel na simu zote clone nazo zina hii chipset za mtk

  1. Anza kwa kuandaa mazingira ya kuflash simu yako ambayo labda iko bricked, au ina tatizo lolote kama hii yangu iliyokuwa inajirestart muda wote
    vitu unavyohitaji ni

a. Drivers za simu (Kama chip yako ni MT65xx family Download Hapa )
b. Smart Phone flash tool (SP Flashtool) Download Hapa
c. MTK Droid Tools Download Hapa
d. ROM / kwa Simu za TECNO karibia zote Zinapatikana Hapa  (hakikisha ni rom sahihi kwa model ya simu yako) Rom za Simu Nyingine kama za clone za MTK zote  Download Hapa

2. Tuanze sasa
a. Chomeka simu yako na iache ifanye installation ya driver zote, kama inazingua install  driver link ziko hapo juu(kama simu yako ni mt65xx)

1

b. NB: Kwa simu za clone huwa hazijulikani model maana zina imitate original, basi tutatumia MTK droid tool kujua model ya simu yetu. fungua application na uiache italeta details zote kuhusu simu

Tayari taarifa za simu tumezipata , kinachofuata hapo ni kudownload firmware specific kwa ajili ya simu yetu. ROM/firmware zipohapo juu(mda mwingine ili kudownload huwa inakubidi ujisajili kwanza) pia unaweza kugoogle ROMs za simu yako kama link zangu huelewi. Hakikisha una extract na ndani kuwe na faili MT(model ya simu yako)_Android_scatter.txt (hakikisha kuna neno scatter kwenye jina la hilo file)

d. Hapo sasa kila kitu tunacho tunaweza kuanza kuflash simu yetu…
e. Ichomoe simu, kisha fungua SP flash flash tools

2

f. Sehemu ya scatter-loading file weka lile .txt file nililokwambia limo kwenye folder uliloextract kule juu

Pia nenda options > usb mode iwe ticked pia hapohapo kwenye options angalia DA download all > Speed > force high speed inakuwa checked

g. Click download kisha iache (usichomeke simu kwanza mpaka imalize) ikimaliza chomeka simu bila betri ukisikia mlio wa simu imekuwa connected kwenye pc haraka rudisha betri bonyeza “firmware -> upgrade” kisha tulia itaanza kuflash simu

3

h. Kama kila kitu kimeenda sawa utaona progress kwa rangi ya njano kama kuna makosa itatokea rangi nyekundu na maelezo

4

Ikikamilisha successiful, itaonesha kiduara cha kijani

Hapo sasa unaweza chomoa simu yako na kuiwasha na utaona inaanza kama mpya vile….

Ukipenda unaweza kuiroot, kubadili IMEI, kuondoa application za kichina zote kwa kutumia MTK Droid tools

#ff0000;">TAHADHARI: SITAHUSIKA NA UHARIBIFU WA KIMAKOSA WA SIMU YAKO, DO AT YOUR OWN RISK

Tufuatilie @MtaawaSaba ili usipitwe na Habari, Uchambuzi na Makala mbali mbali ya mitandadoni na ya kiteknolojia kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Google+ na Youtube, Pia usisite kutoa maoni yako hapo chini au tuandikie barua pepe kwa mhariri@mtaawasaba.com

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
1 Comment

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive