Serikali ya Tanzania kuanza kukusanya kodi kwenye mitandao ya kijamii

Mwandishi Alexander Nkwabi
Serikali ya Tanzania kuanza kukusanya kodi kwenye mitandao ya kijamii, ameyasema hayo leo, Jumatano, Septemba Mosi, 2021 Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba wakati akizungumzia marekebisho ya tozo katika miamala ya simu yaliyofanywa na Serikali. Akifafanua amesema wako kwenye mchakato wa kuanza kutoza kodi makampuni yenye  mitandao ya kijamii kama nchi zingine zinavyofanya.

 Biashara zinahamia kidijitali, kuna ‘components’ kubwa inayofanya biashara kwa njia za kimtandao. Zile biashara zilizohamia kwenye mtandao hakuna eneo zinazotozwa kodi.

Dk Nchemba amesema, “tozo sio adhabu bali ni mshikamano kwa sababu kuna watu wetu wana uhitaji, nilivyoingia niliwaambia watalaamu mbona haya makubwa makubwa tunayaacha? Kwa hiyo tunaangalia namna hivi App vikubwa vikubwa ambavyo tukishika simu zenu mnavitumia, jamaa anakusanya fedha huko huko hapa hana ofisi.

“Au mnaviona vipo katika simu tu, kuna majamaa yanatengeneza fedha, si mmeshavielewa kila kimoja? Ukiondoa vile vyenye namba ya simu vile vingine ambavyo ukibonyeza unaweza kucheza au muziki subscribe. Vipo vingi lakini kodi yake imelipiwa wapi,”amesema Dk Mwigulu.

Dk Nchemba amesema ameshazungumza na wataalamu wake, kuhusu suala hilo na kwamba  wanalilia ‘timing’ hata kama wahusika hawana ofisi hapa nchini,  lakini kwa kuwa  teknolojia inakua hawatashindwa kuwapata hata mahali.

“Biashara zinahamia mtandaoni, tunataka tuone namna ya kupata hii huduma ya kodi kwa njia ya mtandao. Nimewaambia waendelea kuangalia nchi zilizofanikiwa ili tuone namna ya kuichukua.

chanzo: Serikali kusaka kodi za wamiliki wa mitandao

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
1 Comment

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive