Samsung Experience 9.0 yaja na maboresho ya Emoji

Mwandishi Alexander Nkwabi

Kutegemeana na aina ya simu unayotumia, utagundua kuwa kuna tofauti katika Emoji zinazopatikana, ni utaratibu wa kawaida kwa watengenezaji wa simu kutengeneza Emoji za kipekee ili kujitofautisha na simu pinzani. Kwa upande wa Samsung tunaweza kusema wametumia vibaya uhuru huu kwa kutengeneza Emoji za tofauti sana ambazo zimekuwa zikileta mkanganyiko mkubwa kwa watumiaji wa Emoji izo.

Hata hivyo, katika sasisho kubwa la Android Oreo  ambalo Samsung wameachia siku kadhaa zilizopita kuna mabadiliko kadhaa ambayo yamefanyika. Kwa kawaida Samsung na watengenezaji wa simu wengine hutoa matoleo ya Android yakiwa na muonekano wa kitofauti kwa kuongeza au kupunguza baadhi ya vitu kutoka kwenye toleo la stock Android.

Katika toleo hili jipya la Android, Samsung wametoa Samsung experience 9.0 (zamani ikiitwa TouchWiz) ambayo katika maboresho waliyoongeza ni marekebisho ya Emoji. Emoji nyingi kwenye simu za Samsung zimekuwa tofauti na simu zingine, na hivyo kuleta mkanganyiko kwa watumiaji. Mabadiliko hayo ya Emoji yameonekana katika Maktaba ya Emoji (mabadiliko kutoka Samsung Experience 8.5 kwenda Samsung Experience 9.0)

Mfano mzuri wa Emoji iliyokuwa ikileta utata ni ile ya “rolling eyes” ambayo uwa inaonesha mtu anaezungusha macho kama ishara ya kutofurahishwa au kutoridhika na jambo. Katika picha hapa chini utaona kwenye Samsung experience 8.5 emoji imezungusha macho lakini uso unaokana kama unatabasamu tofauti na Emoji inavoonekana na simu au huduma za makampuni mengine.

 

Samsung_experience_9_0_emojipedia_comparison_rolling_eyes_1

Cha kuvutia zaidi, sio maboresho Emoji iyo ya “rolling eyes” tu yaliyofanyika, bali kuna maboresho mengine kama;

Imp-emoji-840x298Samsung-experience-9-0-emojipedia-comparison-faces-tilt-removed-840x298Samsung-drool-face-840x298Grimace-emoji-840x298

Cha kupendeza zaidi ni mabadiliko ya muonekano wa Cookie ambapo mwanzo ilionekana kama biskuti

Samsung-experience-9-0-emojipedia-cookie-1

Mwisho kabisa, kuna emoji mpya nyingi za kutosha zilizoongezwa kwenye Samsung Experience 9.0.  Unaweza kuangalia Emoji mpya zote hapa, japo kuna emoji nyingi pia mabazo hazijafanyiwa mabadiliko yoyote.

Emoji hizi mpya zitaanza kuonekana kwenye simu za Galaxy S8/S8+ ambazo zitapokea sasisho jipya la Android Oreo naSamsung Experience 9.0, na pia tunatarajia kuziona kwenye simu mpya ya Galaxy S9 ambayo tunatarajia itazinduliwa siku zijazo mwezi huu wa pili katika maonesho ya MWC 2018 huko Barcelona Hispania.

Endelea kuwa nasi na usiache kutufuatilia kwenye mitandao mbali mbali kijamii ili usipitwe na Habari, Uchambuzi na Makala mbali mbali za kiteknolojia. kwenye FacebookTwitterInstagram, Google+ na Youtube, Pia usisite kutoa maoni yako hapo chini au tuandikie barua pepe kwa mhariri@mtaawasaba.com

Avatar of alexander nkwabi
Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive