Kila kitu kilichozinduliwa kwenye tukio la Samsung Galaxy Unpacked 2022

Mwandishi Diana Benedict
Leo Kampuni ya vifaa vya kielektroniki ya Samsung imezindua bidhaa kadhaa, na kupitia chapisho hili tutaangazia Kila kitu kilichozinduliwa kwenye tukio la Samsung Galaxy Unpacked 2022.

Uzinduzi huu umelenga mjumuisho wa simu mpya za Samsung Galaxy S22 pamoja na mjumuisho wa tableti mpya za Galaxy tab S8. Ambapo bidhaa zote zimekuja na matoleo matatu huku matoleo ambayo yamepewa jina la Ultra yakipeperusha bendera kwa kubeba sifa za juu kabisa kwenye kikundi cha bidhaa zilizoachiwa leo.

Tukio hili la uzinduzi maarufu kama Galaxy Unpacked lililodumu kwa muda wa saa nzima hufanyika kila mwaka ambapo bidhaa mpya huzinduliwa. Kwa wakati huu hakukuwa na mabadiliko makubwa japo ulikuwa ni uzinduzi wa bidhaa mbili na hakukuwa na mambo mengi zaidi.

Unaweza kuangalia kwa ufupi kilichojiri na bidhaa zilizozinduliwa kwenye video hii hapa chini, ila kuna uchambuzi wa kila bidhaa kwenye machapisho mengine hapo chini.

Galaxy S22 na Galaxy S22 Plus

Galaxy s22 plus

Simu za Galaxy S22 na Galaxy S22 Plus zimejikita zaidi kwenye maboresho ya kamera ikiwemo kuwa na sensa kubwa na uwezo mkubwa wa optical zoom kwenye lenzi za telefoto. Simu hizi zinakuja na chip ya Snapdragon 8 kizazi cha kwanza kwa wateja wa marekani. Pia kioo chake ni kidogo kuliko mtangulizi wake Galaxy S21, upande wa bei za kuanzia ni zilezile, ili kupata uchambuzi wa kina kuhusu simu za Galaxy S22 na Galaxy S22 Plus unaweza kusoma: Kila Kitu Unachotakiwa Kujua Kuhusu Samsung Galaxy S22 Na S22 Plus

Galaxy S22 Ultra

Samsung galaxy s22 ultra

Mabadiliko makubwa mwaka huu ni simu hii imechukua sifa za simu ya Galaxy Note ambayo Samsung wameamua kuiua simu iyo. Simu hii pia inakuja na mabadiliko kadhaa upande wa kamera na uwezo wa kutumia chaja ya 45W. Uchambuzi wa kina zaidi unaweza kuusoma hapa Kila Kitu Unachotakiwa Kujua Kuhusu Samsung Galaxy Tab S8 Ultra

Galaxy Tab S8 na Galaxy Tab S8 Plus 

Tableti za Galaxy Tab S8 na Tab S8 Plus zote zinakuja na S Pen. na  Tab S8 ina kioo chenye ukubwa wa 11-inch LCD na 120Hz refresh rate, wakati Tab S8 Plus inakioo chenye ukubwa wa  12.4-inch OLED. Tableti zote zinakuja na chip ya Snapdragon 8 kizazi cha kwanza. unaweza kusoma zaidi hapa Kila Kitu Unachotakiwa Kujua Kuhusu Samsung Galaxy Tab S8 Na S8 Plus

Galaxy Tab S8 Ultra

Galaxy tab s8

Hii ndioinapeperusha bendera kwa upande wa tableti zilizozinduliwa kwa wakati huu, hii ndio angalau kwa sasa inaonekana kama mshindani anayeeleweka wa ipad Pro kutoka Apple. Kioo chake ni nchi 14.6 inakuja na s pen, ina kamera mbili za mbele kwa ajili ya simu za video. Soma zaidi kuhusu tableti hii hapa: Kila Kitu Unachotakiwa Kujua Kuhusu Samsung Galaxy Tab S8 Ultra

 

Avatar of diana benedict
Mwandishi Diana Benedict Mwandishi
Mitandao ya Kijamii
Diana Benedict. Digital Creator | IT Specialist | Graphics Designer | Web Designer | Web SEO | Contents Management | UI/UX Designer and Social Media Management.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive