Simu isiyoingia maji ya Sony Xperia Z

Imeandikwa na Alexander Nkwabi
Sony Xperia Z

Habari njema kwa watu wote, kampuni ya sony wamezindua simu isiyoingia maji, simu iliyopewa jina la Sony Xperia Z inaweza kuzamishwa mpaka futi 3 chini ya maji kwa muda wa mpaka nusu saa bila kuharibika

Watengenezaji wake waliijaribu bafuni, simu zingine kama iphone huaribika haraka iwapo zitaingia maji au kudondoshwa. Sony Xperia Z imefunikwa kwa kioo kinachokunjika na kuzuia kuvunjika, lakini chembamba kwa milimita 7.9
simu hiyo ilizinduliwa kwenye Consumer Electronics Show (CES) huko Las Vegas,

Sony Xperia Z

simu hiyo pia ina kamera ya hali ya juu yenye – 13 megapixels, yenye nguvu kuliko ile ya iPhone 5 ambayo ni 8 megapixel pekee.

simu hiyo inayotumia android, ina uwezo kuongeza maisha ya betri kwa kuzima programu zisikuwa na umuhimu kwa wakati huo.
pia ina mfumo wa intanet wa 4G connection,na inchi 5 Full HD 1080p.

jiunge nasi kupitia youtube channel yetu

Maoni 2