Simu janja ya Huawei 4Afrika yawasili Afrika

Imeandikwa na Alexander Nkwabi
Huawei 4Afrika

Kampuni ya Huawei kutoka China imeunganisha nguvu na Microsoft ili kuuza “simu janja” ambapo wamedai ndio soko la simu za mkononi linalokua zaidi duniani.

Simu Janja Ya Huawei 4Afrika Yawasili Afrika

Makampuni hayo mawili yameizindua simu iitwayo Huawei 4Afrika Jumanne iliyopita. Simu hiyo inatumia Windows Phone 8 na inakuja na aplikesheni maalumu kwa ajili ya soko la afrika.

Simu Janja Ya Huawei 4Afrika Yawasili Afrika

kwa mujibu wa GSM Association,Afrika ndio soko kubwa la pili baada ya asia na ndio soko la simu za mkononi linalokua kwa haraka zaidi duniani.
Simu hiyo itapatikana kwa kuanzia katika nchi za Angola, Egypt, Ivory Coast, Kenya, Morocco, Nigeria na Afrika ya kusini baadae mwezi huu.

tufuate kwenye mitandao ya kijamii na youtube

Acha Ujumbe