Kampuni ya Uganda yazindua simu mpya ya Android – Mara X

Mwandishi Diana Benedict

Mara Corporation Limited (MC)kampuni kutoka Uganda imeungana na Goolgle kuzindua simu ya Android One iitwayo Mara X, kwa soko la Afrika , tukio hilo limetokea huko MOBILE WORLD CONGRESS, Hispania, Machi 1, 2018. Mara X itakuwa ni smartphone bora Afrika ukilinganisha na TECNO au infinix.

Mara X smartphone

 

Mara X itakuwa ni simu ya kwanza Africa iliyopewa Mfumo wa Uendeshaji wa Android 8.0 kwa kutumia mfumo mpya kabisa wa ulinzi kutoka Google wa Android One na itaweza kupata masasisho ya usalama mpya kutoka Goole kila yatokapo kwa muda wa miaka miwili. Pia Mtumiaji wa Mara X atapata uhifadhi wa picha zenye ubora wa hali ya juu na wa bila kikomo kwenye  kwenye cloud za Google Photos.  “Nchini Afrika na katika masoko mengine mbali mballi duniani yanayoibuka, tunahitaji simu za mkononi ambazo zina bei nafuu sana na za ubora stahiki,” alielezea Mwenyekiti wa Mara Group Jagdish Thakkar. “Simu hizi zinawapa watu uwezo wa kuboresha maisha yao kwa njia ya kupata taarifa mtandaoni na kuitumia kwa huduma za biashara na fedha.” Aliongeza.

Siya Chug, Mkurugenzi wa Brand hiyo, anaelezea Mara Group ilianza kama biashara ndogo ndogo nchini Uganda, na sasa imeongezeka hadi kundi la uwekezaji wa sekta mbalimbali ambalo leo, lina Watu zaidi ya 14,000 katika nchi 25 za Afrika na mabara matatu. Aliongeza na kusema Simu ya Mara X ni simu ya kujivunia kama Brand ya Africa.

Shirika la Mara (Mara.com) linalenga pia kujenga mazingira ya biashara ya digital marketing ili kukidhi mahitaji yanayoendelea Afrika kote kwa kuwekeza katika biashara muhimu kama teknolojia ya kifedha, vyombo vya habari vya kijamii, vifaa mbalimbali na simu kama ilivyoanza na mara X.

 

 

“Mara X ni simu ambayo watu wanaweza kujifurahisha, na kujifunza mambo mbali mbali ya teknolojia. Afrika inaonekana kizazi kipya cha wajasiriamali kutafuta teknolojia ya simu ya mkononi ili kusaidia kuendesha biashara zao za kila siku, na Mara X itawafanyia kazi ili kufuata viwango vya juu zaidi vya utengenezaji wa simu. Bara yetu inatarajiwa kuwa na simu za mkononi zaidi ya milioni 700 ndani ya miaka michache, na uhusiano huo utabadilisha maisha ya waafrika wengi. “- Alisema hayo Mwanzilishi wa Mara Mara, Ashish J Thakkar (AshishJThakkar.com).

Unaweza ku Pre-Order simu ya Mara X hapa

Uchambuzi kamili, ubora, Specifications na bei ya simu hii utakuja mara punde mtaawasba itakapofanikiwa kuipata simu hiyo kwahiyo endelea kuwa nasi pia Subscribe katika chanel yetu ya YouTube kwa makala mbali mbali kila wiki na uchambuzi wa vifaa mbali mbali vya kiteknolojia. usisahau kkuacha maoni yako hapo chini au tutmie barua pepe mhariri@mtaawasba.com

Mwandishi Diana Benedict Mwandishi
Mitandao ya Kijamii
Diana Benedict. Digital Creator | IT Specialist | Graphics Designer | Web Designer | Web SEO | Contents Management | UI/UX Designer and Social Media Management.
1 Comment

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive