Tovuti 5 za kutembelea kama unatafuta ajira Tanzania (2023)

Mwandishi Emmanuel Tadayo
Changamoto ya upatikanaji wa Ajira Tanzania 2022 imekuwa kubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma, hivyo zoezi la kutembea na bahasha ya khaki kutoka ofisi moja hadi ingine imekuwa ni changamoto kubwa ingine.

Hapa ndio unapokuja umuhimu wa tovuti za ajira Tanzania, Tovuti hizi zinakuleta mtafutaji wa ajira karibu na waajiri mbalimbali kuanzia mashirika binafsi, taasisi za serikali na kadhalika na kurahisisha zoezi zima la utafutaji ajira.

Kama unatafuta ajira Tanzania 2022, kuna tovuti nyingi ambazo zimejikita katika kuunganisha watafuta ajira na waajiri ambazo zitakusaidia kutafuta ajira kutokana na utaalamu na uzoefu wako.

Makala hii inakuletea tovuti 5 za ajira Tanzania 2022 ambazo ni za uhakika katika kukusaidia kukukutanisha na waajiri mbalimbali.

Ajira Leo

Tovuti hii huchapisha nafasi mpya za ajira kila siku kutoka kwa waajiri mbalimbali nchini, Pia tovuti hii huchapisha nafasi za scholarships kutoka nchi mbalimbali, nafasi za internship pamoja na admission za vyuo mbalimbali nchini. Kama wewe ni mtafutaji wa ajira na unataka ajira kwa haraka basi hakikisha unatembela tovuti hii kila siku.

Ajira yako

Tovuti hii hukuleta karibu mtafutaji wa ajira na waajiri mbalimbali ikiwemo makampuni mbalimbali nchini Tanzania Pamoja na taasisi za ki serikali na zile zisizo za serikali. Nafasi za ajira hutangazwa kila siku hivyo kuleta urahisi wa kujua kazi husika imetangazwa lini, na kama muda wa tangazo hilo umeisha au la. Cha kufurahisha ni kwamba matangazo haya ya ajira ni bure kabisa na usikubali kulipa mtu yoyote ili kupata nafasi za ajira zinazotangazwa kwenye tovuti hii ya Ajira Yako

Ajira zetu

Tovuti hii inafanana kwa namna nyingi na hizo juu, ambapo tovuti hii itakuwezesha kutafuta ajira kutoka makampuni na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali ambazo  hutangaza nafasi za ajira kila siku kupitia tovuti hii. Pia ikiwa mtu ana maswali kuhusu jambo lolote, baada ya kufungua tovuti hiyo huwa kuna ujumbe unakuja ambao humuwezesha mtu kuuliza na kujibiwa maswali moja kwa moja mara baada ya kuandika jina na barua pepe yake.

Brighter  Monday (Zoom Tanzania Jobs)

Tovuti hii ni moja ya tovuti kubwa na ni bure kabisa kwa watafuta ajira, itakukutanisha na waajiri mbalimbali ikiwemo mashirika na makampuni ya binafsi. Tovuti hii itakutaka kutengeneza profile ambayo utaweka taarifa zako ikiwemo CV na taarifa zako za elimu, ujuzi wako na machaguo mengine kuhusu ajira unayohitaji. Utakuwa ukipokea ujumbe kwa njia ya barua pepe kila nafasi ya ajira inayofanana na vigezo vyako inapochapishwa.  Pia tovuti hii huchapisha ushauri, mbina na mengine mengi kuhusu ajira na utafutaji wa ajira kwa ujumla

Empower

Tovuti hii inafanana kwa kiasi kikubwa na Brightermonday. Tovuti hii itakutaka kutengeneza profile ambayo utaweka taarifa zako ikiwemo CV na taarifa zako za elimu, ujuzi wako na machaguo mengine kuhusu ajira unayohitaji. Utakuwa ukipokea ujumbe kwa njia ya barua pepe kila nafasi ya ajira inayofanana na vigezo vyako inapochapishwa.  Pia tovuti hii huchapisha ushauri, mbina na mengine mengi kuhusu ajira na utafutaji wa ajira kwa ujumla

Pia unaweza tembelea hizi;

Jobs Today (Tanzania)

Jobs Today ni tovuti nyingine ambayo ni bora kwa ajili ya kufauta nafasi za kazi hapa nchini Tanzania, tovuti hii ni kama tovuti nyingie zilizo tangaulia lakini hii ina angazia zaidi kwenye mchanganyiko wa ajira pamoja na elimu kwa nchini Tanzania. Kupitia tovuti hii hutaweza kuangalia nafasi mpya za kazi kila siku, pamoja na nafasi za scholarships, na admission.

Mabumbe

Tovuti hii inakuletea nafasi za ajira kutoka nchini Tanzania na nchi zingine za Jirani kama Kenya na Zambia kila siku, pia wanakuletea nafasi za scholarship kutoka nchi mbalimbali.

Udahili Portal

Udahili Portal ni tovuti nyingine ambayo ni bora kwa ajili ya kufauta nafasi za kazi hapa nchini Tanzania, tovuti hii ni kama tovuti nyingie zilizo tangaulia lakini hii ina angazia zaidi kwenye mchanganyiko wa ajira pamoja na elimu kwa nchini Tanzania. Kupitia tovuti hii hutaweza kuangalia nafasi mpya za kazi kila siku, pamoja na nafasi za scholarships, na admission.

Hitimisho

Kupitia mtandao wa intaneti  wengi wamepata ajira rasmi na zisizo rasmi. Hivyo ni muhimu kupitia tovuti, blogu, mitandao ya kijamii kama instagram, facebook, LinkedIn na kadhalika ili kuweza kupata kazi ambayo unaweza kuimudu kulingana na ujuzi na utaalamu ulio nao.

Pia ni vyema kwa muombaji wa ajira kuwa na nyaraka muhimu zinazoweza kuhitajika kwa haraka kama vile kitambulisho cha kitaifa kinachotolewa na NIDA, na vyeti vya kuhitimu masomo au ujuzi mbalimbali alionao muhusika ili kurahisisha mchakato wa uombaji ajira katika taasisi,mashirika na kampuni mbalimbali kwa urahisi.

Mtaawasaba inakutakia utafutaji mwema wa ajira kupitia mtandao wa intaneti. Pia usisahau kutembelea mitandao yetu ya kijamii instagram, twitter na Facebook, pia tembelea na utufuate kwenye channeli yetu ya YouTube

Avatar of emmanuel tadayo
Mwandishi Emmanuel Tadayo Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
mwandishi wa habari za teknolojia kwenye tovuti pendwa ya mtaawasaba
7 Comments

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive