Tweet ya Kylie Jenner yagharimu SnapChat Dola bilioni 1.3

Mwandishi Alexander Nkwabi

Siku ya alhmisi ilikuwa mbaya baada ya hisa za Snapchat kuporomoka ghafla na kampuni iyo imepoteza karibu dola za kimarekani billioni 1.3 mpaka 1.6 kwenye soko la hisa baada ya mwanadada Kylie Jenner ambaye ni  maarufu kwenye reality show ya Keeping Up With The Kardashians, kuandika tweet inayosema hatumii tena mtandao wa kijamii wa Snapchat.

Kylie Jenner ambae akaunti yake ya Snapchat ndiyo inayotazamwa kuliko zingine zote, ni mmoja wa watu mashuhuri wenye ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.Kilichomfanya aandike hivyo ni baada ya kutofurahishwa na mabadiliko makubwa ya muonekano wa SnapChat ambao umelalamikiwa na watumiaji kuwa mgumu kutumia.

Snapchat ambayo kwa sasa inakumbwa na ushindani mkubwa kutoka kwa App zingine za mitandao ya kijamii inayohusisha kushea picha kama Instagram.

Sio Kylie Jenner pekee ambaye amelalamikia mabadiliko ya muonekano bali, watumiaji wengi wamekuwa wakilalamikia mabadiliko hayo yaliyofanywa siku za hivi karibuni. Ukitazama maoni ya watumiaji kwenye App Store na Google Play utaona malalamiko mengi ni kwa sababu ya mabadiliko ya muonekano. Baadhi ya watu wanakusanya sahihi milioni 1.2 za watumiaji kwenye  Change.org wakiomba SnapChat warudishe muonekano wa mwanzo.

Kujibu malalamiko hayo, Snap Inc. ambao ndio wanaosimamia mtandao huo wa kijamii walisema; “Tunaelewa sana mabadiliko haya mapya ya Snapchat hayakuwafurahisha wengi”

“Kwa kuweka kila kitu kuhusu marafiki zako pamoja, lengo letu ni kukufanyia urahisi kuungana na wale uwapendao”

Wakaongeza kuwa: “Msingi huu mpya ni mwanzo tu, tutaendelea kuwasikiliza kwa ukaribu na kutafuta njia mpya kufanya huduma zetu kuwa bora kwa kila mmoja”

Hata hivyo mwanadada Kylie Jenner baadae aliandika tweet ingine siku iyo iyo akisisitiza kuwa hata hivyo bado anaipenda na ataendelea kuipenda SnapChat

Endelea kuwa nasi kwa kutufuata kwenye mitandao ya kijamii, na usisahau ku subscribu ili uwe wa kwanza kupata Habari, Uchambuzi na Makala mbali mbali z kisayansi na teknolojia. Pia usisahau ku acha maoni yako hapo chini na unaweza kuwasiliana nasi kwa barua pepe mhariri@mtaawasaba.com

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive