Ubora wa Apple iPhone 8, 8 Plus na iPhoneX

Mwandishi Diana Benedict

Utangulizi

Septemba 12 mwanzoni mwa mwezi huu kampuni ya Apple imezindua simu zake tatu ambazo ni iPhone 8, iPhone 8 Plus na iPhoneX ijulikanayo kama (iPhone 10), simu zote tatu zitauzwa kwa makadirio ya kuanzia 699$ (sawa na shilingi 1,565,760) kwa iPhone 8, 799$ (sawa na shilingi 1,789,760) kwa iPhone 8 Plus na 999$ (sawa na shilingi 2,23,760) kwa iPhoneX. Hapa tutaangazia muonekano, na bora wa Apple iPhone 8, 8 Plus na iPhoneX;

Muonekano

Ubora wa Apple iPhone 8, 8 Plus na iPhoneX iPhone 8 na iPhone 8 Plus zimeundwa kwa alluminium body zenye kuwekwa kioo katika shepu yake ya nyuma na zote zinapatikana kwa machanganuo ya rangi ya silver (nyeupe) gold na spacegrey.

iPhone 8 ni ndogo kwa umbo na nyepesi yenye milimita za msitatili 138.4 x 673 x 7.3mm na yenye uzito wa gramu sizizozidi 148g, wakati iPhone 8 Plus yenyewe ni kubwa kuzidi iPhone 8 yenye milimita za msitatili 158.4 x 781 x 7.5mm na yenye uzito wa gramu zisizozidi 202g.

iPhoneX yenyewe haijatofautiana sana na iPhone8 na 8Plus, imeundwa kwa aluminium boby lakini yenyewe yenye kamera mbili nyma zilizosimama tofauti na iPhone 7 Plus na 8 Plus na kwa zinapatikana kwa rangi mbili tu ambazo ni Silver na Spacegrey, kwa ukubwa iPhoneX ina milimita za msitatili 143.6 x 709 x 7.7 na uzito wa gramu zisizozodi 174g,

Simu zote tatu zinatumiamfumo mmoja wa system charge (Apple lighting USB) na pia hazina port ya headphone jack kama walivyofanya klatika toleo lao lililopita la iPhone 7 na 7 Plus.

iPhone 8 ina lensi moja ya kamera (back camera) yenye uwezo wa Megapixel 12 wakati iPhone 8 Plus na iPhoneX zote zinatumia mifumo ya camera mbili za nyuma yenye uwezo kurekodi 4k videos.

Ulinzi

Kwa upande wa iPhone 8 na iPhone 8 Plus zenyewe zinatumia mifumo ya ulinzi ile tuliyoizoea kama iliyopo kwenhye matoleo ya simu zilizopita kama iPhone 5s, 6, 6Plus, 6s, 6sPlus, 7 na 7Plus (TouchID) kwa simu za Android kama Samsung tunauita FingerPrind ID  iliyopo mbele chini ya kioo katika uso wa simu. Lakini Tukitazamia katika upande wa Device hii mpya iPhoneX yenyewe haitumia mfumo wa TouchID by the way inatumia mfumo mpya unaouitwa FaceID, sio mgeni sana katika technogolia tukikumbuka mwaka 2015 samsung wao walishaunda katika program yao ya android  aina hii ya ulizi, (Tutautazamia Zaidi katika Makala ijayo mfumo huu wa faceid kwa unda usikose)

Ubora wa Apple iPhone 8, 8 Plus na iPhoneX

Display

Apple iPhone 8 ina ukubwa wa inch 4.7 LED-Backlit retina HD Display yenye resolution ya 1334 x 750 Pixel ni sawa ukilinganisha za matoleo ya iPhone 6, 6s na 7.

Apple iPhone 8 Plus yenyewe ina ukubwa wa wa inch 5.5 7 LED-Backlit retina HD Display yenye resolution ya 1920 x 1080 Pixelsawa na ukubwa wa iPhone 6Plus, 6sPlus na 7 Pluskatika matoleo ya zamani ya iPhone.

Kwa upande wa iPhoneX yenyewe imekuja kuwa tofauti kidogo yenye kioo kikubwa na resolution kubwa Zaidi ikilinganishwa na simu zote hapo juu ina ukubwa wa inch 5.8 edge-to-edge OLED Super Retina screen 2436 x 1125 (4k) yenye kioo kilichopinda katika kona zake zote nne inayofanya kuongea uzuri wa simu uwe wa kuvutia Zaidi yenye mwanga unaoendana na mazingira uliyopo iwe ya jua kali au mwanga Hafifu.

Camera

Unapozungumzia ulimwengu wa smartphone basi lazima uiangalizie na ubora wa camera unaopatikana katika simu hiyo,

Apple iPhone 8 ina camera moja nyuma yenye uwezo wa Megapixel 12 yenye uwezo wa kuekodi mpaka resolution ya 4k na megapixel 7 za camera ya mbele kwa ajili ya selfie, facetime na videocall,

iPhone 8 Plus na iPhoneX zenyewe zina camera mbili nyuma zenye uwezo sawa japo katika Ubora wa Apple iPhone 8, 8 Plus na iPhoneXiPhone 8 Plus ikiwa na camera ya kulala na iPhoneX ikiwa ya kusimama, zote mbili hizo zina uwezo wa megapixel 12 back dual camera, ambapo camera ya pili inasupport kuzoom zidi ya 10x, Camera ya mbele haikutofautina na ile ya iPhone 8 ambayo ina megapixel 7 za camera ya mbele kwa ajili ya selfie, facetime na videocall.

Hardware, Specification na Software

Simu zote tatu zimettengenezwana Processor mpya kabisa kutoka Apple ziitwazo A11

Ubora wa Apple iPhone 8, 8 Plus na iPhoneX

Bionic Chip, kwa upande wa iPhone 8 ina 1821mAh za battery na uwezo wa 2gb ya Ram, iPhone 8 Plus ina 2675mAh za battery na uwezo wa 3gb ya ram, Bado hatujapata data kamili kuhusu uwezo wa battery ya iPhoneX lakini yenyewe ina uwezo wa 3gb Ram pia zikiwa zinasupport wireless fast charging tofauti na model za iPhone zilizopita!

Simu zote tatu zinakuja na iOS 11 pre-installed OS kama iPhone Operating System (iOS) na zimegawanyika katika ukubwa wa 64gb ya storage na 256gb tu tofauti na zile za mwanzo kama iphone 7 yenye 32gb, 128gb.

hitimisho

Kwa sasa bado hatujapata bei kamili ambazo tungewezakukadiria kuuzwa katika soko la Tanzania, endelea kuwa nasi tulendelee kukupa updates Zaidi za kiteknolojia pia usisahau kututembelea katika social network kama Instagram, facebook na twitter @MtaaWaSaba

 

 

Mwandishi Diana Benedict Mwandishi
Mitandao ya Kijamii
Diana Benedict. Digital Creator | IT Specialist | Graphics Designer | Web Designer | Web SEO | Contents Management | UI/UX Designer and Social Media Management.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive