Uzinduzi wa iPhone 13: Jinsi ya kufatilia mubashara kwenye Apple event

Imeandikwa na Alexander Nkwabi
Uzinduzi Wa Iphone 13: Jinsi Ya Kufatilia Mubashara Kwenye Apple Event
Leo usiku tarehe 14, kutakuwa na Uzinduzi wa iPhone 13 pamoja na bidhaa zingine kutoka kampuni ya Apple. kupitia chapisho hili tunakuelekeza Jinsi ya kufatilia mubashara Apple event kupitia njia mbalimbali. Twende moja kwa moja kwenye njia hizo.
  1. Kupitia YouTube

hii ndio njia rahisi zaidi kutumia popote pale ulipo duniani cha muhimu uwe na mtandao wa internet tu. Unaweza kufalia mubashara kwa kubofya kitufe hapa chini au kwenda YouTube kwenye channel ya Apple.

2.  Ukurasa wa Apple Event

unaweza pata tukio zima mubashara kwa kubofya kiunga cha Apple events na moja kwa moja utaweza kutazama tukio hilo

 

Muda wa kuanza Apple Event

Kwa watazamaji walio Tanzania na nchi za jirani, tukio litaanza kuoneshwa mubashara kuanzia saa mbili kamili usiku za afrika ya mashariki

 

Tutarajie nini

unaweza soma chapisho letu linaloonesha ni yapi mazuri tunayotarajia kutoka Apple, bofya hapa kusoma chapisho hilo

Acha Ujumbe