The Wall: TV yenye ukubwa wa ajabu kutoka Samsung

Mwandishi Alexander Nkwabi

Ni mashindano ya nani mwenye uwezo kutengeneza Televisheni kubwa, ambapo siku kadhaa kabla ya maonesho ya CES 2018 kuanza kampuni ya LG ilionesha TV yake kubwa kabisa yenye ukubwa wa inchi 88. Leo Samsung wamekuja na Televisheni kubwa kabisa ya 4K waliyoipa jina la The Wall, yenye ukubwa inchi 146 na teknolojia ya MicroLED.

The Wall TV 2018

Samsung wameitaja kama ndio Modular Tv ya kwanza duniani ambapo TV ndogo ndogo zinaweza unganishwa pamoja kupata moja kubwa. Televisheni hii inatumia teknolojia ya MicroLED ambayo inafanana kwa ukaribu na teknolojia ya OLED.

Kwa sasa TV iko katika hatua ya Concept na bado haijaanza kutengenezwa kwa ajili ya matumizi ya watu wote, Samsung wamesema kutakuwa na uzinduzi wa dunia nzima siku itakapotoka miezi kadhaa ijayo mwaka huu.

Endelea kutembelea tovuti ya Mtaawasaba ili upate kujuzwa mambo mbalimbali yanayotokea huko Las Vegas kwenye Maonesho ya CES 2018

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive