WhatsApp inafanya majaribio ya malipo kwa sarafu za kidigitali

Imeandikwa na kasomi
Whatsapp Inafanya Majaribio Ya Malipo Kwa Sarafu Za Kidigitali

Miezi sita iliyopita kampuni ya Meta ilitoa Wallet yake ya sarafu za kidigitali ambayo inaitwa Novi Wallet na inatumia Stablecoin ya Pax Dollars (USDP) ambayo ni crypto yenye thamani sawa na Dola 1.

WhatsApp imeanza majaribio ya kuunganisha Wallet ya Novi na WhatsApp hivyo utaweza kutuma na kupokea pesa moja kwa moja katika WhatsApp kwa kuunganisha Wallet ya Novi na app yako ya WhatsApp.

Majaribio hayo yameanza kwa watumiaji wa Marekani ikiwa ni sehemu ya kujaribu mfumo na kucheck utaratibu wa kupata vibali na kupima mfumo. Mfumo wa WhatsApp hauna makato katika mihamala!

Signal pia imeweka uwezo wa kutuma Crypto na ipo katika majaribio. Apps nyingi zinapambana kuweka urahisi huo ili kutangulia mbele katika ulimwengu wa malipo ya mitandao na umiliki wa fedha za kidigitali.

Acha Ujumbe