YouTube kuonesha bure zaidi ya vipindi 4000 vya runinga vikiwa na matangazo

Mwandishi Alexander Nkwabi
Kupitia chapisho kwenye blogu ya YouTube limeandikwa, sasa YouTube kuonesha bure zaidi ya vipindi 4000 vya runinga vikiwa na matangazo, na kukufanya uendelee kufuatilia mtandao.
Watazamaji wataweza kutazama vipindi vya runinga kama vile vipindi vya mapishi kama Hell’s Kitchen cha Gordon Ramsey, Unsolved Mysteries, na Sanctuary. Katika tangazo lililoachiwa na YouTube, wanasema wataleta msisimko wa kipekee kwani vipindi vingi vitaoneshwa kwa video zenye ubora wa 1080p na sauti yenye ubora wa 5.1 surround.

Utaratibu huu sio mgeni kwani unaonekana ni ule tuliozoea miaka na miaka tunavoangalia vipindi kwenye king’amuzi ambapo huwa na matangazo katikati ya vipindi. Kwa miaka mingi YouTube imekuwa ikitumia matangazo kwenye video zinazooneshwa bure kwenye mtandao huo, kwa sasa wamepiga hatua zaidi.

YouTube pia wataonesha filamu zaidi ya 1,500 kutoka kwa wasambazaji wakubwa wa filamu duniani kama Warner Bros., Paramount Pictures, na Disney, pamoja na maelfu ya vipindi kutoka kwa wasambaji hao ambapo vipindi vipya vitakuwa vinaongezwa kila wiki kuanzia siku vinapoanza kuoneshwa.

YouTube kuanza kutoa huduma hii ya kuonesha vipindi vya runinga bure ni sehemu tu ya maboresho, ambapo pia tumeona wakianzisha YouTube Shorts ili waweze shindana na TikTok. Unaweza Tembelea ukurasa wa Filamu na Michezo ya kuigiza ili uweze kuona filamu na michezo ya kuigizwa inayowekwa na YouTube

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive