Kuhusu Sisi

Tangu mwaka 2012, tovuti ya Mtaawasaba ni  chanzo cha kuaminika kwa  wasomaji wetu kufanya maamuzi sahihi ya machaguo yao kupitia Habari, mitazamo, uchambuzi na video mbalimbali za bidhaa za kielektroniki ambazo tunadhani ni za muhimu kwa watumiaji. Tunahakikisha machapisho yetu yanapitiwa na wahariri wetu kabla hayajakufikia msomaji wetu mpendwa.

 

lengo letu ni kuhakikisha unakuwa wa kwanza kupata habari, makala, uchambuzi wa teknolojia

 

Kwa mwezi tuna wastani wa wasomaji takribani 10,000. Pia tuna mamia ya wafuasi kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram, Facebook, Twitter na chaneli yetu ya YouTube. Timu yetu: Mtaawasaba inaendeshwa na timu ya waandishi, wahariri, na wachambuzi mahiri katika maswala ya teknolojia. Unaweza kuilewa vizuri timu iliyo nyuma ya pazia la Mtaawasaba kwa kutembelea ukurasa wa waandishi. Na kwa maelezo mbalimbali, kutuma Habari, au kutaka kuwa mchangiaji wa Makala hapa Mtaawasaba, unaweza kutembelea ukurasa wetu wa mawasilianoWaandishi wa Mtaawasaba ni pamoja na;

  • Joeli, Muanzilishi na msimamizi mkuu
  • Kato Kumbi, Mwandishi mkuu na mchambuzi
  • Emmanuel Tadayo, Mwandishi
  • Hemedans Nassor, Mchambuzi, Mchangiaji
  • Hassan Kabelwa, Mchangiaji
 

Kama unadhani unaweza kuandika kwa ajili ya Mtaawasaba, usisite bofya hapa kuwasiliana nasi

Historia

Tovuti hii ilianzishwa Novemba 2012 na Joeli, mshabiki na mwandishi wa maswala yahusuyo teknolojia. Ilianza kufanya kazi rasmi mwaka 2013 mwezi wa pili. Mtaawasaba.com na sehemu ya mtandao wa tovuti zinasimamiwa na kampuni ya midia ya Mtaawasaba Interactive.

Unahitaji kuwasiliana nasi?

Tunapenda kusikia kutoka kwako msomaji wetu. Una taarifa unataka kutupa? Maswali au maoni kwa timu ya Mtaawasaba? Tuandikie kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano ili utoe yako ya moyoni. Matangazo, Leseni, na Ruhusa kutumia machapisho? Kama unapenda kutangaza kupitia Mtaawasaba.com ama unahitaji ruhusa kutumia machapisho yetu, tafadhari wasiliana nasi kupitia ukurasa wa ruhusa na matangazoUngependa kuwa mwandishi wa Mtaawasaba? Kama unaamini una uwezo wa kuandika vizuri kuhusu teknolojia hasa kuhusu gajeti, softiwea na mengine yahusuyo teknolojia, kwa nini usifikirie kuwa sehemu ya timu ya Mtaawasaba? Tuandikie kwa barua pepe au jaza fomu ya kwenye ukurasa wetu wa mawasiliano

 
Kuhusu sisi
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive