Best Tech Blogs in Tanzania (2024) Updated

Alexander Nkwabi 86

Unatafuta blogu za teknolojia nchini Tanzania? Usihangaike zaidi! Mtaawasaba imeandaa orodha ya tovuti bora zilizojikita kwenye uwanja wa teknolojia, hasa kwa watumiaji wa lugha ya kiswahili.

Ikiwa wewe ni mpenzi wa teknolojia anayevutiwa na maendeleo ya hivi karibuni katika sekta ya teknolojia ya Tanzania, Afrika na duniani kote kwa ujumla, hakikisha unaangalia tovuti hizi. Tovuti hizi zina utajiri wa habari juu ya startups, ujasiriamali, vidokezo juu ya mada mbalimbali, fedha, na rasilimali.

Kwa hiyo hebu tuanze na kupitia blogu za teknolojia kutoka nchini Tanzania (bila mpangilio maalum).

1. Teknokona (www.teknolojia.co.tz)teknokona

Teknokona, moja ya tovuti kongwe za habari na mafunzo ya teknolojia nchini Tanzania. Hapa utapata makala za kuvutia na zenye manufaa kuhusu matumizi ya teknolojia katika maisha yako ya kila siku. Pia wanakuletea habari za hivi karibuni kuhusu bidhaa mpya, huduma, na maendeleo katika sekta ya teknolojia, bila kusahau mafunzo ya jinsi ya kutumia teknolojia kwa njia bora na salama. ili kukufanya uwe na ujuzi na uzoefu wa teknolojia ambao utakusaidia kuboresha maisha yako na kuchangia katika jamii yako.

 

2. Mtaawasaba (www.mtaawasaba.com)mtaawasaba screenshot

Mtaawasaba.com tovuti namba moja kwa habari, makala, na uchambuzi wa teknolojia kwa watumiaji wa lugha ya Kiswahili, imekuwepo kuanzia mwaka 2013, ikikuletea habari na makala, pia imekuwa ikichambua bidhaa za teknolojia ikiwemo simu za mkononi, tableti, kompyuta, programu na mengi yahusuyo teknolojia. Tovuti hii inaandikwa na timu ya waandishi wenye uzoefu na weledi katika fani zao. Unaweza acha maoni, ushauri na michango ili kuboresha huduma zao. Tunatumaini utafurahia kusoma mtaawasaba.com!

 

3. Tanzania Tech (www.tanzaniatech.one)

tanzaniatech

Tanzaniatech.one ni moja ya tovuti maarufu Tanzania inayotoa habari, uchambuzi na maoni kuhusu teknolojia, biashara na ubunifu nchini Tanzania. Lengo lao kubwa ni kuwaelimisha, kuwahamasisha na kuwawezesha watanzania kufaidika na fursa zinazotokana na teknolojia. Wanafanya hivyo kwa kutoa makala, video, podcast na matukio mbalimbali yanayohusu teknolojia kwa lugha ya kisswahili na kiingereza.

 

4. SwahiliTek (www.swahilitek.com)

swahilitek

Swahilitek.com ni tovuti mpya inayotoa habari na mafunzo kuhusu teknolojia mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili. Lengo la tovuti hii ni kuwawezesha watu wanaozungumza Kiswahili kufahamu na kufaidika na teknolojia za kisasa, kama vile kompyuta, simu, intaneti, programu, roboti, na kadhalika. Tovuti hii pia ina jukwaa la majadiliano ambapo watumiaji wanaweza kushirikiana na kubadilishana uzoefu na maarifa kuhusu teknolojia. Swahilitek ilianza kwa kuchapisha machapisho yake kupitia mitandao ya kijamii hasa instagram.

 

5. HabariTech (Habaritechtz.com)

Habaritechtz.com ni tovuti inayokuletea habari na makala za kiteknolojia kwa lugha ya Kiswahili. Lengo lao ni kukujuza na kukuelimisha kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu teknolojia, kama vile simu, kompyuta, programu, mitandao, usalama na mengineyo. Kama una shauku ya teknolojia na unapenda kujifunza zaidi, karibu ujiunge na habaritechtz.com leo!

 

 

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive