Google I/O 2022: Pixel 6a, Pixel Watch, na kila kitu kilichotangazwa leo

Mwandishi Alexander Nkwabi
Leo ni siku lile tukio la kila mwaka ambapo Google hukutana na ma developer kwa ajili ya matangazo na uzinduaji wa bidhaa na huduma kwa mwaka husika. Mwaka huu, Google I/O 2022 kumekuwa na uzinduzi wa bidhaa kadhaa ambazo baadhi zimekuwa zikitajwa kwenye tetesi kwa muda.

Kama kwa sababu yoyote hukuweza kufuatilia mkutano huo wa masaa mawiili, usihofu tutapitia kitu kimoja kimoja ambacho kimezinduliwa leo. Bila kupoteza muda tuanze na bidhaa ya kwanza

Google kuja na saa janja ya Pixel Watch

2022 5 11 google io 840 11 28 51
kwa hisani ya : Google

Baada ya tetesi kwa muda sasa na picha kadhaa za inayodhaniwa kuwa ni saa janja ya Pixel, hatimaye leo Google wamethibitisha kuwa watazindua saa janja ya Pixel Watch kipindi cha majira ya pukutiko mwaka huu. Saa hii janja ndio itakuwa ya kwanza kabisa kutengenezwa na Google. Hii ni baada ya kuinunua kampuni ya Fitbit.

Hakuna maelezo zaidi kuhusu saa hii janja zaidi ya picha za awali zilizovuja, hata hivyo Google wameachia picha rasmi ya saa hii. Maelezo zaidi yasome hapa

Google yatangaza simu za Pixel 7 na Pixel 7 Pro

Pixel 7 and Pixel 7 Pro
kwa hisani ya : Google

Google pia wametangaza simu mpya ambazo zitakuwa mrithi wa simu zilizozinduliwa mapema mwaka huu. Wametengaza kuja na simu za Google Pixel 7 na Pixel 7 Pro. Kuhusu bei na tarehe ya kuzinduliwa haijatajwa ila tunachojua mpaka sasa ni, simu hizi zitakuja na mfumo endeshi wa android 13, pia zitakuwa na toleo jipya la chip ya Tensor. Kimuonekano zimefanana sana na simu za Pixel 6. Kujua zaidi unaweza pitia makala hizi.

Simu ya Google Pixel 6a kuingia sokoni hivi karibuni

2022 5 11 google io 762 11 31 34
kwa hisani ya : Google

Pia Google wametangaza simu ya bei nafuu kiasi ya Pixel 6a, simu hii inafanana kwa kiasi kikubwa na pixel 6 itaingia sokoni kwa bei ya dola za marekani 500. Kioo chake ni inchi 6.1 kwa upana , ram ndogo kidogo ya Pixel 6, na chip ya Tensor sawa na simu za Pixel 6 na 6Pro. Isome stori hii kwa urefu hapa

Google Pixel Buds Pro zinakuja kwa dola 200

Pixel Buds Pro 1 1
kwa hisani ya : Google

Pixel Buds pia zimetangazwa. Hizi ni wireless earphones ambazo zitaingia sokoni kwa bei ya dola 200 za marekani, Zinakuja na uwezo wa kuzuia vumbi na jasho na hivyo kufaa kwa mazoezi. Unaweza soma kwa kirefu zaidi kuhusu Pixel Buds hapa

Google warudi na Pixel Tablet

Pixel Tablet
kwa hisani ya : Google

Baada ya kuacha kwa miaka kadhaa , hatimaye Google wamerudi tena kwenye utengenezaji wa tableti. “Pixel Tab” hii inaweza ingina sokoni mwaka 2023. Hakuna maelezo mengine ya zaidi.

Google Pay sasa kuwa Google Wallet

Google wamekuwa wakitoa huduma ya kuhifadhi kadi zako kwa ajili ya kufanya manunuzi bila kutumia kadi. Huduma hii iliyojulikana kama Google Pay sasa iankuwa Google Wallet, sasa utaweza kuhifadhi kadi zako za benki, vitambulisho, tiketi za matamasha, kadi za chanjo na zaidi. upatikanaji wa huduma hii itategemeana na nchi uliyopo.

Android 13 Beta 2 rasmi leo

io2022 beta oems android 13
kwa hisani ya : Google

Imekuwa wiki chache tu tangu beta ya kwanza ya Android 13 ilipozinduliwa, lakini tayari tunapata beta mpya – na wakati huu, inakuja na watengenezaji wa wahusika wengine. Karibu kampuni kadhaa, pamoja na OnePlus, Lenovo, na zaidi, ziko kwenye bodi na uboreshaji wa leo.

Google kuja na Miwani janja ya AR

Screen Shot 2022 05 11 at 12.13.12 PM

Google ilikuwa na habari moja zaidi kabla ya kumalizai. Kampuni hiyo iliweka wazi kuwa ilikuwa ikifanyia kazi jozi mpya ya miwani ya AR iliyoundwa “kuvunja vizuizi vya mawasiliano.” Mfano wa mapema wa Google demoed unaweza kutafsiri lugha inayozungumzwa, kutoa maelezo mafupi ya wakati halisi kwa mvaaji. Google haikushiriki jina la kifaa cha mfano, wala haikusema wakati inaweza kuitoa kwa watumiaji.

Mengineyo

  • Google Assistant kupata maboresho zaidi
  • Google Maps kupata maboresho zaidi
  • Google Translate kuweza kutafsri lugha zaidi
  • Virtual credit cards in Chrome itaweza kutengeneza kadi ya benki ili kulinda kadi halisi ya mtumiaji
Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive