Huawei kuja na P20 iliyo na kamera tatu na notch kama ya iPhone X

Mwandishi Diana Benedict
Ushindani wa display notch bado unaendelea katika smartphones za android kuiga kutoka iPhone X, kampuni kama Asus, Doogee na OnePlus ni kampuni ambazo zimeiga muonekano wa iPhone X na sasa Huawei kuja na P20 iliyo na kamera tatu nyuma na notch juu ya kioo chake.

nexus2cee Screen Shot 2018 03 07 at 5.41.32 PM 2

Kama ninavyosemaga, ukiiga boresha ndicho ninachokiona kwa simu mpya ya Huawei P20 inayotarajiwa kuzinduliwa hivi tarehe 27 machi 2018. kupitia ukurasa wa Twitter ilitangaza uzinduzi huo wa Huawei P20 kuzinduliwa tarehe hiyo.

https://twitter.com/HuaweiMobile/status/968130704780529665

Muonekano wa Huawei P20
Kabla ya yote simu hizi zinatarajiwa kuwa Tatu amabzo ni Huawei P20 ya kawaida, Huawei P20 Pro na Huawei P20 Lite. Huawei zote zinakuja na rangi za  Ceramic Black / Twilight, Midnight Black / Klein Blue na Sakura Pink.

Huawei P20 Lite 2

Vyombo vya habari mabli mbali vinathibitisha kwamba simu ya Huawei P20 Lite na ya kawaida zitakuja na kamera tatu za nyuma ambayo moja yake ikiwa chini ya wide angle, na Fingeprint iliyowekwa nyuma katikati. Pia hatutaraji kuona jackphone ya kichwa cha 3.5mm katika Huawei P20,na badala yake itakuwa na USB-C ambayo ndio kiunganishi cha sauti na data zote kama ilivyo iPhone X.

Kutoka kwenye picha tunaweza kuona bezels nyingi sana na skrini ya ukubwa wa mtindo. Ingawa iPhone X ina uwiano wa screen wa 19.5: 9,  lakini kwa Huawei P20 itakuwa na ratio ya screen ya 18.7: 9. simu ambayo itakuwa na kioo cha HD nadhani zaidi hata ya iPhone X.

dims

Huawei P20 Specification
Tunatarajia kuona Huawei P20 kuongozwa na Chipset ya Kirin 970, ambayo pia ilikuwa kwenye Huawei Mate 10 ambapo hii imeboreshwa zaidi ya mara 25 kutoka ile ya kwanza. Kirin 970 ni chip ya octa-core (4×2.4GHz Cortex-A73 na 4×1.8GHz coresx-A53 cores) iliyojengwa na GPU 12 zenye cores zilizojengwa kwenye mchakato wa 10nm.

Hizi ni baadhi ya Specification zitakazokuwa ndani ya simu zaidi utazipata simu itakapozinduliwa.

 • Kirin 970 octa-core processor
 • 5.84in Full-HD+ (2280×1080) ‘notch’ screen
 • 4GB/6GB RAM
 • 64GB/128GB storage + microSD
 • Leica 12Mp + 20Mp kamera mbili na moja ya ziada
 • kamera ya mbele ni 16MP
 • Fingerprint scanner ya mbele kwa P20 ya kawaida na fingerprint ya nyuma kwa P20 Lite
 • Betri ya 3320mAh
 • USB-C
 • Android 8.0 Oreo
 • Ukubwa wa
 • 148.6×71.2×7.4mm na uzito wa 145g

Haijathibitishwa zaidi simu hizi zitauzwa kwa kiwango gani, mpaka hapo zitakapotoka, Endelea kutufutilia mtaawasaba chanzo chako cha habari za kuaminika uendelee kupata habari za teknolojia.

Mwandishi Diana Benedict Mwandishi
Mitandao ya Kijamii
Diana Benedict. Digital Creator | IT Specialist | Graphics Designer | Web Designer | Web SEO | Contents Management | UI/UX Designer and Social Media Management.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive