Waliojitangaza kutoa huduma ya Starlink wakamatwa Dar-Es-Salaam

Amos Michael Maoni 35

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam likishirikiana na kikosi kazi maalum cha kuzuia na kupambana na makosa ya kimtandao limewakamata watu wawili, Claudian Makaranga (28) mkazi Kawe, na Hongliang Yang (35) mwenye asili ya china, mkazi wa Kigamboni, kwa tuhuma za kuingiza vifaa vya mawasiliano ya intaneti nchini bila kufuata utaratibu wa kisheria vyenye jina la STARLINK KIT/DEVICE.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda maalum SACP Jumanne Muliro anasema Watuhumiwa hao wamekuwa wakijitangaza kuuza vifaa na kutoa huduma ya internet nchini Tanzania kupitia mtandao ya kijamii wa Instagram kwa akaunti yenye jina la STARLINK.

Baadhi ya vifaa vya Starlink vilivyokamatwa ni Starline Dish 12 na Starlink Router 12, akifafanua zaidi alisema, baadhi ya vifaa vilivyoingizwa nchini imebanika vilishauzwa na kutumika katika baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam kitendo ambacho ni kosa na kinyume na sheria kwani havijaidhinishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Aidha ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na matumizi ya vifaa vya mawasiliano, ambavyo havijaidhinishwa na mamlaka husika.

Februari 26, 2024, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, kupitia Mtandao wa X (Twitter) alisema Kampuni ya Starlink inayotoa Huduma za Intaneti kwa kutumia ‘Satelaiti’ inakamilisha hatua za mwisho ili kupata vibali vya kutoa Huduma Nchini.

 

MADA:
Mwandishi Amos Michael Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
Meezy ni mchangiaji wa machapisho mbalimbali hapa Mtaawasaba tangu kuanzishwa kwake. Meezy ni mpenzi wa Android na anapokuwa nyumbani hupendelea kupiga kinanda na kuandaa muziki
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive