MtaawasabaMtaawasaba
  • Habari
  • Simu
  • Android
  • Kompyuta
  • Windows
  • Maujanja
  • StartUps
Mengineyo
  • Muongozo
  • Maujanja
  • Programu
  • Simu Janja
  • Teknolojia
Mtaawasaba
  • Kuhusu Sisi
  • Sera ya faragha
  • Vigezo na Masharti
  • Wasiliana Nasi
Mitandao
  • Facebook
  • Twitter
  • Instagram
  • YouTube
  • Newletters
© 2013 - 2023 Mtaawasaba Interactive
Unasoma Starlink kuanza kutoa huduma za intaneti Tanzania robo ya kwanza 2023
MtaawasabaMtaawasaba
  • Apple
  • kompyuta
  • Maujanja
  • Apps
  • StartUps
  • Magari
  • Mtaawasaba
    • Habari
    • Makala
    • Apps
    • Maujanja
    • Kompyuta
    • Simu Janja
    • Magari
    • Matukio
    • Muongozo wa mtumiaji
    • Mitandao ya kijamii
    • Programu
    • Teknolojia
    • Mfumo endeshi
    • Miwani Janja
    • Saa Janja
    • Televisheni
    • Utamaduni
  • Mengineyo
    • Microsoft
    • intaneti
    • Windows
    • SnapChat
    • TTCL
    • Tigo Tanzania
    • vifurushi visivyo rasmi
    • Google
    • halotel
    • Instagram
    • iOS
  • Kuhusu Mtaawasaba
    • Kuhusu Sisi
    • Sera ya faragha
    • Vigezo na Masharti
    • Wasiliana Nasi
Una akaunti? Ingia
Tufuate mtandaoni
© 2022 Mtaawasaba Interactive. Haki zote zimehifadhiwa.
Mtaawasaba > Habari > Starlink kuanza kutoa huduma za intaneti Tanzania robo ya kwanza 2023

Starlink kuanza kutoa huduma za intaneti Tanzania robo ya kwanza 2023

Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) imethibitisha kuwa Kampuni ya Starlink inatafuta kibali cha kuzindua huduma za intaneti za satelaiti nchini.

Imeandikwa na Emmanuel Tadayo Miezi 4 iliyopita
Sambaza
Starlink kutoa huduma za internet Tanzania

Kampuni ya Starlink inayotoa huduma za intaneti kupitia satelite, yenye makao makuu yake makuu huko Hawthorne, California, inatarajiwa kuanza kutoa huduma za intaneti nchini Tanzania kuanzia robo ya kwanza ya mwaka 2023, huduma hii ya intaneti ya kasi inatarajiwa kuongeza kasi ukuaji wa uchumi wa kidijitali nchini.

Bilionea Elon Musk ambaye ndiye mmiliki wa Starlink, Tesla, SpaceX na sasa mmiliki wa Twitter, kupitia tovuti ya Starlink amesema amevutiwa na mazingira ya uwekezaji Tanzania na kampuni yake ya Starlink itafanya uwekezaji mkubwa kuanzia Mwaka 2023 endapo atapata kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Unaweza Kusoma

Elon Musk ametangaza rasmi vita na Apple

Ramani, kutoka Tanzania yakusanya $32m kurahisisha mnyororo wa usambazaji

Teknolojia ya hali ya juu kutumika katika Kombe la Dunia la FIFA Qatar 2022

Tovuti ya iCloud ya Apple yapata muonekano mpya, inavutia zaidi.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabiri Bakari amethibitisha kuwa kampuni hiyo ya Starlink ilituma maombi ya kutoa huduma ya intaneti nchini kupitia tovuti ya TCRA.

SpaceX ambayo ni kampuni mama Ilianzishwa mwaka 2002 na bilionea Elon Musk kwa lengo lililoelezwa la kupunguza gharama za usafiri wa anga za juu ili kuwezesha watu kufika Sayari ya Mars.

Kampuni hii ambayo inajinadi kutoa intaneti ya kasi duniani kote, mpaka kufikia Juni 2022 imeripoti kuwa ina wateja zaidi ya 500,000 katika nchi 40. Mpaka sasa mataifa pekee ya Afrika ambayo yameanza kupata huduma za intaneti kutoka Starlink ni Nigeria na Msumbiji.

Hali ya upatikanaji wa Intaneti nchini Tanzania

Kwa mujibu wa ripoti ya robo ya nne ya mwaka 2021 kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), takwimu zinaonesha kuwa Watumiaji wa intaneti nchini Tanzania ni takribani milioni 29.8 ambao ni ongezeko  la asilimia 4.4 kutoka idadi ya Watanzania milioni 28.5 kwa mujibu wa takwimu za robo ya mwisho ya mwaka 2020.

Zaidi ya asilimia 90 ya Watanzania wanapata huduma ya intaneti kupitia simu zao za mkononi, na ingawa bei za data za simu za mkononi ziko chini (ukilinganisha na nchi zingine), bado hazijapatikana kwa bei nafuu kwa makundi ya watu ambao wengi wao wanaishi vijijini, na kusababisha pengo kubwa la matumizi ya intaneti kati ya mijini na vijijini.

 

KWENYE Elon Musk, intaneti, Starlink, tanzania
Sambaza chapisho hili
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Telegram Barua Pepe Nakili kiungo Durufu
Acha Ujumbe

Toa Jibu Ghairi kujibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Mtaawasaba Newsletter

Jiunge nasi kwa njia ya barua pepe tukujulishe kila inapotoka habari mpya

Zaidi Kutoka Mtaawasaba

Sasa unaweza pata Blue Tick kwa kulipia Instagram na Facebook

Sasa unaweza pata Blue Tick kwa kulipia Instagram na Facebook

Siku 4 zilizopita
Airtel yawa ya kwanza kuzindua huduma ya kadi za eSIM Tanzania

Airtel yawa ya kwanza kuzindua huduma ya kadi za eSIM Tanzania

Siku 5 zilizopita
Instagram yazindua Notes, Candid Stories, na Zaidi

Instagram yazindua Notes, Candid Stories, na Zaidi

Miezi 3 iliyopita
Umoja wa Ulaya waishinikiza Apple kuruhusu maduka mbadala ya programu kwenye iPhones na iPads

Umoja wa Ulaya waishinikiza Apple kuruhusu maduka mbadala ya programu kwenye iPhones na iPads

Miezi 3 iliyopita

© 2013 - 2023 Mtaawasaba Interactive. Crafted by Simba Creative

  • Kuhusu Sisi
  • Sera ya faragha
  • Vigezo na Masharti
  • Wasiliana Nasi
Go to mobile version
logo logo
Karibu Mtaawasaba!

Jaza taarifa kuingia Kwenye Akaunti Yako

Umesahau Nywila?