Watumiaji wa intaneti wazidi kuongezeka Tanzania 2021

Mwandishi Alice
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wametoa ripoti ya takwimu mpya za robo ya nne ya mwaka 2021, takwimu hizo zinaonesha kuwa Watumiaji wa intaneti wazidi kuongezeka Tanzania kufikia milioni 29.8 mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2021 ambalo ni  sawa asilimia 4.4 kutoka milioni 28.5 kwa mujibu wa takwimu za robo ya mwisho ya mwaka 2020..

watumiaji wa intaneti 2021

ongezeko hilo la watumiaji wa intaneti ni takribani asilimia 50 ya idadi ya watanzania wote kufikia mwaka 2021 ukilinganisha na mwaka 2020 ambapo ongezeko lilikuwa ni asilimia 49.

watumiaji wa intaneti 2021 2

Ripoti hii iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  inaonesha kuwa idadi ya watumiaji wa simu za mkononi imeongezeka na kufikia watumiaji milioni 54 kutoka watumiaji milioni 27.62 kwa mwaka 2012,  mtandao wa simu wa Vodacom Tanzania ukiongoza kwa kuwa na watumiaji waliojisajiliwa 15,913,553 wakifuatiwa na Airtel kwa kuwa na watumiaji waliosajiliwa 14,700,426. Hata hivyo idadi hii imepungua ukilinganisha watumiaji mwanzoni mwa robo ya 4 ya 2021 ambapo jumla ya watumiaji ilikuwa 54,514,544 ukilinganisha na mwishoni mwa robo 54,116,216.

watumiaji wa mitandao ya simu 2021 2

unaweza isoma ripoti kamili hapa

Mwandishi Alice Mhariri Mkuu
Mitandao ya Kijamii
Alice ni mwandishi na mhariri wa makala mbalimbali hapa Mtaawasaba tangu mwaka 2016. Akiwa hayupo kazini hupendelea kusoma vitabu, kuogelea na kusikiliza muziki
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive