Internet Explorer yapumzishwa baada ya miaka 27

Mwandishi Emmanuel Tadayo

Hatimaye, Internet Explorer yapumzishwa baada ya miaka 27. Kampuni kubwa ya teknolojia ya Microsoft rasmi “imestaafisha” kivinjari chake cha wavuti cha Internet Explorer kuanzia leo Jumatano. “e” ya bluu na nyeupe, wakati mwingine ikiwa na utepe wa dhahabu, itakuwa inaacha kufanya kazi kwenye kompyuta duniani kote, na mtandao.

Internet Explorer yapumzishwa baada ya miaka 27

Baada ya miaka ya 27 ya kutamba, hatimaye leo Microsoft wanapumzisha kivinjari cha wavuti cha Internet Explorer na mbadala wake utakuwa ni kivinjari cha Microsoft Edge ambacho kwa mujibu wa Microsoft kinadaiwa kina usalama zaidi na kiko fasta zaidi. Internet Explorer kwa miaka kadhaa imekuwa ikihusishwa na mapungufu ya kiusalama kwa watumiaji wake.

Kwa wavuti na programu za zamani ambzo hutegemea kivinjari cha Internet Explorer,au kwa namna moja au ingine ukiwa una hitaji kutumia kivinjari hiko kinachopumzishwa leo, unaweza tumia Edge ina kipengele cha “Internet Explorer mode”.

Matumizi yoyote ya programu ya Internet Explorer (IE) yatakupeleka kwenye kivinjari cha Mcrosoft Edge na utapewa ujumbe utakaokujulisha kuwa Edge ina kasi zaidi na ni salama zaidi kwa matumizi.

Kifo cha Internet Explorer hakijaja tu ghafla, kwani kwa miaka sasa kivinjari hiki kimekuwa kikijikongoja dhidi ya washindani wake kama vile Google Chrome, Mozilla Firefox, na hata kivinjari cha Microsoft cha Chromium-based Edge. Matumizi ya Internet Explorer yamepungua katika miaka ya hivi karibuni, na kwa mujibu wa ripoti ya StatCounter inaonyesha IE ina chini ya nusu ya jumla ya sehemu ya soko la kivinjari.

Baada ya hapo Microsoft ikaonelea iongeze kipengele cha “Internet Explorer mode”  katika kivinjari cha Edge na kuwahimiza watumiaji wa Windows kuhamia kwenye Edge kabla ya kufunga programu asili ya Internet Explorer kwa kompyuta za mezani.

 

 

Mwandishi Emmanuel Tadayo Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
mwandishi wa habari za teknolojia kwenye tovuti pendwa ya mtaawasaba
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive