Kampuni ya Sony imezindua Dolby Vision Blu-ray player na Dolby Atmos receiver

Imeandikwa na Kato Kumbi
Kampuni Ya Sony Imezindua Dolby Vision Blu-Ray Player Na Dolby Atmos Receiver

Kampuni ya Sony imezindua 4K Blu-ray Player ambayo inasupport Dolby Vision HDR na A/V receiver ambayo inatoa audio ya Dolby Atmos huko kwenye maonesho CES 2018. Blu-ray Player ya UBP-X700 imeundwa kwa ajili ya diski za Blu-ray za 4K ikiwa ni pamoja na HDR10 au Dolby Vision na inajumuisha programu za Netflix, Amazon Prime Video na YouTube.

Kampuni Ya Sony Imezindua Dolby Vision Blu-Ray Player Na Dolby Atmos Receiver
The STR-DH790 receiver,

Na Receiver ya STR-DH790, kulingana na Sony inaweza kupitisha muundo wote wa HDR bila kupoteza ishara yoyote. Bidhaa zote mbili zimezinduliwa iki ni pamoja na televisheni ya hivi karibuni iliyozinduliwan na kampuni hiyo ya Sony. Mtaawasaba.com bado haijapata bei kamili ya bidhaa hizo japo bidhaa hizo zitaingia sokoni hivi karibuni.

Pia kampuni ya Sony imezindua bidhaa zingine ikiwemo simu tatu Sony Xperia XA2, XA2 Ultra pamoja na L2. Mbwa Roboti anajulikana kama AIBO na bidhaa zingine kadhaa.

Acha Ujumbe