Samsung wana uwezo wa kuzima TV zilizoibiwa.

Mwandishi Alexander Nkwabi

Samsung wana uwezo wa kuzima TV zilizoibiwa. ambapo TV yoyote ya Samsung inaweza kuzimwa kwa kutumia teknolojia iliyomo ndani ya TV hizo.  Hii imekuja baada ya uporaji wa TV za Samsung huko Afrika kusini.

Wiki kadhaa zilizopita kulitokea machafuko huko Afrika kusini ambapo waandamanaji walivamia maduka na kupora bidhaa zenye thamani Zaidi ya mamilioni ya dola. Moja ya walioathirika na dhahama hii ilikuwa na ghala la Samsung lililoko maeneo ya pwani ya mashariki ya Afrika kusini ambapo TV kadhaa mpya ziliporwa na waandamanaji hao.

TV nyingi zilizoporwa zimeonekana zikiuzwa mitaani kwa bei sawa na bure, bila wahalifu hao kujua kama Samsung wana mbinu zao za kuwadhibiti.

Kwa kutumia teknolojia ya TV Block, Samsung wameanza kuzizimisha TV zote zilizoporwa. Hii ilifahamika kufuatia Habari kwa waandishi iliyotolewa mapema mwezi hu una Samsung huko Korea ya kusini kufuatia uporaji huo.

Teknolojia hii ya TV Block ni mfumo wa usalama wa TV za Samsung ambapo mtumiaji wa mwisho aliyepata TV hiyo kwa njia zisizo halali atashindwa kuitumia pindi tu atakapomaliza kuisaji kabla hajaanza kuitumia.

TV Block ni nini?

Kwa mujibu wa Samsung, TV Block ni mbinu ya ulinzi inayofanya kazi kichinichini ambayo inagundua kama kifaa husika kimewashwa, na kuhakikisha kifaa hicho kinatumika na mmiliki wa halali mwenye Ushahidi wa umiliki wa kifaa hicho.

 

Teknolojia hii ipo kwenye TV zote za Samsung ikiwa na lengo la kudhibiti soko la kati kama lile la wauzaji wa bidhaa zilizoibiwa duniani kote.

Akizungumza bwana Mike Van Lier, ambaye ni mkurugenzi wa bidhaa za kielektroniki afrika kusini alisema, “In keeping with our values to leverage the power of technology to resolve societal challenges, we will continuously develop and expand strategic products in our consumer electronics division with defence-grade security, purpose-built, with innovative and intuitive business tools designed for a new world. This technology can have a positive impact at this time, and will also be of use to both the industry and customers in the future.”

Samsung TV Block inafanyaje kazi?

Mtu mwenye TV iliyoibiwa anapoiunganisha kwenye internet wakati anaisajili, namba za usajili za TV hiyo zitagundulika na seva ya Samsung. Hii itaamsha mfumo wa uzimaji iyo TV na kuizuia kufanya kazi

Na kama itatokea mtu aliyenunua kwa halali TV yake na ikajifunga wakati anaisajili, Samsung wamehakikisha TV za namna hiyo zitarudishwa kawada pindi tu atakapoonesha Ushahidi wa kuinunua TV hiyo kutoka kwa wauzaji wanaotambuliwa.

Je, naweza tumia Samsung TV Block iwapo TV yangu itaibiwa?

Jibu ni la, kwa sasa Samsung wamesema wanaweza kuzuia TV nyingi zinazoibiwa kwa mara moja na sio moja moja, japo tunatarajia kuiona teknolojia hii ikifaa hata kwa mtu mmoja mmoja. Nadhani watanzania wengi wataifurahia huduma hii pindi itakapoachiwa kwa watu wote.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive