Kufa kwa symbian neema kwa asha sasa yapata multitasking na swipe ui

Mwandishi Hemedans Nassor

wengi wetu tunazijua simu za nokia asha kama feature phone simu ambazo ni ndogo na zisizo na nguvu, lakini mambo yamebadilika sasa nokia wameijenga upya operating system yao ya asha (Nokia Asha software platform 1.0). operating system hii sasa imeekwa test ya meego kama vile nokia n9. na sasa ina uwezo wa kufungua application nyingi kwa wakati mmoja (multitasking).

nokia-unveils-asha-501-at-99-to-take-on-googles-android-based-phones

vitu muhimu vya kuangalia kwenye hii operating system mpya ya asha.

ulaji wa battery

operating system hii inaonekana ni nyepesi sana kwani simu iliyozinduliwa nayo asha 501 ina battery yenye ukubwa wa 1200mah lakini imeweza kukaa na chaji siku 48 bila kutumiwa ikiwa on tu na masaa 17 ya kuongea. hii inamaana asha hii inakaa na chaji kuliko kisimu cha tochi ambacho kinakaa na chaji hadi siku 35

 

specification za simu

mpaka sasa ipo simu moja tu yenye network ya 2g double line, haina specific za kutisha ina ram 64mb na internal 128mb lakini hili haliifanyi hii simu iwe slow, simu ipo fasta kama smartphone nyengine. nokia wameahidi itatoka version ya pili yenye speed ya 3g na specification kubwa

nokia-asha-501-color-range

 

multitasking

hichi ndio kitu muhimu zaidi kilichokua kinsubiriwa na wengi kwa nokia asha kua na multitasking. asha sasa inauwezo wa kufungua application nyingi kwa mpigo. mfano kuacha browser inadownload huku unasoma document huku unaskiliza mziki kwa wakati mmoja.

 

homescreen mpya

kwenye hii asha os mpya kuna homescreen za aina mbili, ya kwanza ni menu na ya pili ni fastlane. ngoja niielezee fastlane kidogo hii ni homescreen ambayo utaona open application utaona activities za jana utaona na za leo na utaeka za kesho kama unataka.

Nokia-Asha-501-one-swipe-jpg

 

general user interface

muonekano wa asha wote umebadilika, kuanzia music player, video player na sehemu za kuandikia text kama message. now kwenye asha unaweza kueka image ndo ikawa background ya menu na pia cha muhimu zaidi ni swipe ui. kama upo familia na meego utakuwa unajua kua n9 haina button hata moja kila kitu unaswipe. kwenye asha kuna button moja tu kila kitu kinafanywa kwa kuswipe.

 

video

kama hujaridhika na maneno kuna video nzuri inayoonyesha hii simu unaweza iangalia hapa

https://youtube.com/watch?v=laIDw78OVjM

 

je unaionaje nokia asha mpya? umeipenda kama mimi? niandikie hapo chini kwenye comments

Mwandishi Hemedans Nassor Mchangiaji
Hemedans aka Chief Mkwawa, amekuwa mwandishi wa makala mbalimbali za teknolojia kuanzia kuanzishwa kwa Mtaawasaba. Kwa sasa ni mchangiaji kila anapopata nafasi
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive