Android 12 imewekwa mfumo wa Android Auto na itakuwa na uwezo wa Digital Car Key

Alexander Nkwabi Maoni 49
Mwaka huu Google ilipofanya presentation kuhusu maboresho ya Android 12; moja kati ya sifa mpya ya Android 12 ni uwezo wa kutumia NFC na Ultra-Wideband (UWB) kuunganisha na mifumo ya magari.

Android 12 imewekwa mfumo wa Android Auto na itakuwa na uwezo wa Digital Car Key ambayo inawezesha watumiaji kuwasha gari, kuzima, na ku-lock gari ambazo zinakubali mfumo wa Digital Key. Brand ya kwanza ya magari ambayo imeanza ushirikiano na Android ni BMW.

• Kuanzia wiki hii, watumiaji wa Google Pixel 6 na Samsung Galaxy S21 series wanaweza kuunganisha Digital Key ya BMW.

Tayari Digital Wallet zimeanza kuweka mfumo wa kuhifadhi vyeti, kadi za benki, vyeti vya chanjo na taarifa za msingi.

Apple ilianza kuweka uwezo wa Digital Car Key kuanzia katika iPhone XS na XR na kuendelea. Ni move ambayo inaelekea kurahisisha matumizi ya Digital Car Keys katika miaka ijayo.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive