‎Apple inaondoa programu ambazo hazijasasishwa kwa muda‎ mrefu

Mwandishi Diana Benedict

Katika juhudi za kuboresha Duka la Programu maarufu kama App Store kuwa rahisi kutumia, ‎Apple inaondoa programu ambazo hazijasasishwa kwa muda‎ mrefu. Taarifa zinasema kuwa Apple inapanga kupiga panga programu zote ambazo hazijasasishwa katika miaka miwili iliyopita.

Apple imeanza kufanyia tathmini programu ambazo inadhani zinaweza kuwa zimepitwa na wakati. Ikiwa programu hizo zitaonekana hazijawahi kusasishwa ndani ya miaka 2, kampuni itawajulisha wasanidi programu husika. Hata hivyo, Apple itaondoa mara moja programu za zamani ambazo hazitasasishwa ndani ya siku 30 baada ya tangazo hili. Baada ya kuondolewa, watumiaji ambao tayari wamepakua programu wanaweza kuendelea kutumia na kuipakua tena. Programu zilizoondolewa pia zitabaki kwenye akaunti za wasanidi programu ili waweze kuweka majina ya programu.

‎The Verge‎ ambao ndio walikuwa wa kwanza kushapisha taarifa hii wameandika‎, watengenezaji wamekuwa wakilalamika kwenye mitandao ya kijamii juu ya sera hii mpya, kwani hii inaweza kuwa na madhara kwa watengenezaji wadogo na wa kujitegemea.

Mwandishi Diana Benedict Mwandishi
Mitandao ya Kijamii
Diana Benedict. Digital Creator | IT Specialist | Graphics Designer | Web Designer | Web SEO | Contents Management | UI/UX Designer and Social Media Management.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive