BasiGo imekusanya dola milioni 6.6 kuleta mabasi ya umeme Kenya

Mwandishi Emmanuel Tadayo

Kampuni inayojihusisha na utengenezaji wa magari ya umeme ya BasiGo, inayofanya shuguli zake nchini Kenya, imekusanya takribani dola za kimarekani milioni 6.6 kuleta mabasi yanayotumia umeme yatakayotumika kwa ajili ya usafiri wa umma nchini Kenya. Kiasi icho kimepatikana kutoka Toyota, kupitia kampuni yake tanzu ya ubia ya Mobility 54.

Toyota ilitoa kiasi cha dola za Marekani milioni 1 kwenye mradi wa BasiGo. Wawekezaji wengine walioshiriki ni pamoja na Novastar; kampuni ya VC inayolenga Afrika na Trucks.vc, kampuni ya VC yenye makao yake Silicon-Valley ambayo inaunga mkono startups katika sekta ya usafirishaji.

Fedha hizi zinatarajiwa kutumika katika kuharakisha juhudi za BasiGo kutengeneza mabasi ya umeme kwa ajili ya usafiri wa umma nchini Kenya na bara la Afrika kwa ujumla.

Toyota imekuwa ikifadhili startups zinazojihusisisha na umeme, baadhi ikiwa ni pamoja na Zembo, mtengenezaji wa pikipiki ya umeme nchini Uganda, na Aceleron mtengenezaji wa betri wa Uingereza.

Inasemekana, mabasi 15 ya umeme ya BasiGo yatawasilishwa mwezi januari 2023 na yataanza kufanya kazi na waendeshaji wengi wakubwa wa mabasi jijini Nairobi.  Kampuni hii inatarajiwa kuweka kuweka miundombinu rahisi zaidi ya kuchaji kote nchini katika kipindi chote cha mwaka 2023. Pia, kampuni hiyo inasema, kuwa inatarajia kuwa na mabasi zaidi ya 1000 ya umeme yanayofanya kazi nchini Kenya ifikapo 2025.

BasiGo itatoa mabasi ya umeme kwa waendeshaji wakubwa wa mabasi nchini Kenya kupitia suluhisho la kipekee la ufadhili wa kampuni ya “Pay-As-You-Drive”, ambalo linawawezesha wamiliki wa mabasi ya umma kununua basi la umeme kwa gharama sawa na basi sawa la dizeli.

 

Avatar of emmanuel tadayo
Mwandishi Emmanuel Tadayo Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
mwandishi wa habari za teknolojia kwenye tovuti pendwa ya mtaawasaba
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive