Ikiwa ni mda mchache tangu fila hii ya Black Panther kuzinduliwa sehemu mbali mbali bado inaendelea kuwa gumzo na kuonekana kuwavutia watu wengi zaidi kuangalia filamu hiyo. Filamu inayohusu mji wa kufikirika wa Kiafrika na imesheheni waigizaji wenye asili ya Afrika.
Wakati filamu hii ikiendelea kuwa Gumzo mmoja wa waigizaji wa Kiafrika Lupita Nyongo alisema hakuwahi kusikia filamu hata moja ya kishujaa yenye watu weusi.
”Tangu mwanzo kabisa wakati Ryan aliponiambia juu ya maudhui ya filamu hii, sikuamini – sikuwahi kuskia hata filamu moja ya ushujaa ya namna hii. Nikamuuliza “Una uhakika Marvel wamekubaliana na simulizi hii? Akasema ndio ndio, wamekubali. Kikubwa katika filamu hii ni kwamba haijaogopa kugusia masuala ya msingi na ya kina ya kijamii na kisiasa na kwa kweli inaendana kabisa na ulimwengu wetu huu wa leo” Alisema hayo Lupita wakati akihojiwa na Mwandishi wa BBC Kim Chakanetsa.
Kwa sasa filamu hiyo imeshaanza kuonesha sehemu mbali mbali hasa ikiwemo hapa Tanzania na inaonesha kuwavutia watu wengi zaidi kutamani kwenda kuitazama filamu hiyo.
Tufuatilie kwenye mitandao mbali mbali ili usipitwe na Habari, Uchambuzi naMakala mbali mbali ya mitanadoni na ya kiteknolojia kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Google+ na Youtube, Pia usisite kutoa maoni yako hapo chini au tuandikie barua pepe kwa [email protected]