MtaawasabaMtaawasaba
  • Habari
  • Simu
  • Android
  • Kompyuta
  • Windows
  • Maujanja
  • StartUps
Mengineyo
  • Muongozo
  • Maujanja
  • Programu
  • Simu Janja
  • Teknolojia
Mtaawasaba
  • Kuhusu Sisi
  • Sera ya faragha
  • Vigezo na Masharti
  • Wasiliana Nasi
Mitandao
  • Facebook
  • Twitter
  • Instagram
  • YouTube
  • Newletters
© 2013 - 2023 Mtaawasaba Interactive
Unasoma Cryptocurrency ni nini?
MtaawasabaMtaawasaba
  • Apple
  • kompyuta
  • Maujanja
  • Apps
  • StartUps
  • Magari
  • Mtaawasaba
    • Habari
    • Makala
    • Apps
    • Maujanja
    • Kompyuta
    • Simu Janja
    • Magari
    • Matukio
    • Muongozo wa mtumiaji
    • Mitandao ya kijamii
    • Programu
    • Teknolojia
    • Mfumo endeshi
    • Miwani Janja
    • Saa Janja
    • Televisheni
    • Utamaduni
  • Mengineyo
    • Microsoft
    • intaneti
    • Windows
    • SnapChat
    • TTCL
    • Tigo Tanzania
    • vifurushi visivyo rasmi
    • Google
    • halotel
    • Instagram
    • iOS
  • Kuhusu Mtaawasaba
    • Kuhusu Sisi
    • Sera ya faragha
    • Vigezo na Masharti
    • Wasiliana Nasi
Una akaunti? Ingia
Tufuate mtandaoni
© 2022 Mtaawasaba Interactive. Haki zote zimehifadhiwa.
Mtaawasaba > Chaguo la Mhariri > Cryptocurrency ni nini?

Cryptocurrency ni nini?

Imeandikwa na Alexander Nkwabi Miaka 5 iliyopita
Sambaza
Cryptocurrency ni nini?
Yaliyomo
Cryptocurrency ni nini haswa?Uvunaji (mining) ni nini?Unaweza kufanya nini na cryptocurrency?Kununua vituKuwekezaUhalali wa cryptocurrenciesFaida na hasara ya cryptocurrenciesCryptocurrencies kubwa unazotakiwa kuzijuaMijadala ya cryptocurrencies?Neno la mwisho

Cryptocurrency sio neno geni masikioni kwako ndugu msomaji. Ni mada ambayo imekuwa ikizungumziwa sana hasa hasa kipindi cha miaka ya hivi karibuni. Lakini je, tunajua cryptocurrency nini? inafanyaje kazi? inapatikanaje? Ungana nami katika makala hii tukiangazia yote kuhusu cryptocurrency.

cryptocurrencies-4

Unaweza Kusoma

Elon Musk ametangaza rasmi vita na Apple

Ramani, kutoka Tanzania yakusanya $32m kurahisisha mnyororo wa usambazaji

Teknolojia ya hali ya juu kutumika katika Kombe la Dunia la FIFA Qatar 2022

Tovuti ya iCloud ya Apple yapata muonekano mpya, inavutia zaidi.

Inawezekana ushawahi kusikia neno cryptocurrency siku zilizopita. Lakini unajua nini kuhusu neno hilo? Cryptocurrency ni nini haswa? Neno hili limeleta mkanganyiko mkubwa kwa wengi hasa kwenye dunia ya kidijitali.

Twende pamoja ili tuweze kuondoa baadhi ya mkanganyiko huu, tumeandaa maelezo ambayo yatakupa mwangaza kuhusiana nayo, inaptikanaje, inafanyaje kazi? faida zake na kadhalika.

Cryptocurrency ni nini haswa?

cryptocurrencies

Kwa maelezo rahisi kabisa Crypocurrency ni mfumo wa kifedha wa kidijitali unaokuruhusu kununua vitu mtandaoni. Ni kama hela hizi za kawaida isipokuwa hizi ni mtandaoni tu, tofauti ya fedha hizi na zile tulizozizoea ni kuwa Cryptocurrency hazisimamiwi wala kumilikiwa na Serikali au benki. Hii ina faida zake na hasara zake ambazo tutazichambua huko chini.

Cryptocurrency au hela ya kimtandao unayomiliki inahifadhiwa kwenye “digital wallet” au kwenye kompyuta iliyo offline au kwenye simu janja yako. Kila muamala wa Cryptocurrency unarekodiwa kwenye blockchain ambapo uko wazi kwa watumiaji wote kuuona.

Uvunaji (mining) ni nini?

Icarus_Bitcoin_Mining_rig-1024x768-1-768x576

Sasa tumeshajua Cryptocurrency ni nini? Swali linalofuata ni inapatikanaje? Cryptocurrencies zinapatikana kwa kuvunwa (mining). Uvunaji huo hufanywa kupitia kompyuta, ambayo hujaribu kufanya mahesabu makubwa na magumu yanayoitwa hash.

Watu dunia nzima wanashindana kuvuna na atakaekuwa mshindi anapata sehemu ya cryptocurrency aliyovuna. Mchakato huu wa uvunaji unahitaji mashine(komyuta) maalumu zinazofanya kazi kutwa kucha.

Uvunaji sio njia pekee ya kupata cryptocurrencies, Njia rahisi ni kununua kupitia wauzaji mbalimbali walioko kwenye masoko ya kuuza na kununua cryptocurrency.

Bitcoin ndio cryptocurrency yenye bei ghali kuliko zote, inauzwa mpaka mpaka shilingi za kitanzania millioni 50 (wakati mada hii ikiandikwa). Na bei yake imekuwa ikipanda na kushuka sana.

Unaweza kufanya nini na cryptocurrency?

Kununua vitu

Zamani ilikuwa ngumu kupata wauzaji wanaokubali kupokea Crypocurrencies kama njia ya malipo. Siku izi imekuwa jambo la kawaida kuona watu mbalimbali wakipokea cryptocurrency.

Kuwekeza

Mwanzoni watu walinunua cryptocurrencies kwa gharama ndogo sana kisha wakaziacha tu. Mara ghafla miaka ya hivi karibuni watu wamekuwa mamilionea kwa fedha zao walizohifadhi miaka iyo na kuzisahau. Mfano Bitcoin ambayo ilikuwa na thamani ya dola za kimarekani 800 kwa bitcoin moja, mwezi wa 11, 2017 ikapanda ghafla na kufikia dola za kimarekani 7000 kwa kila bitcoin.

Uhalali wa cryptocurrencies

Kadri umaarufu wa cryptocurrencies unavozidi ndio vyombo vya sheria na mamlaka za kodi vinajaribu kuelewa namna hizi cryptocurrencies zinavofanya kazi na namna ya kuziingiza kwenye utaratibu wa kila siku wa uhalali kisheria.

Kufikia novemba 2017, matumizi ya Bitcoin na sarafu zingine za kimtandao zimepigwa marufuku kutumika kwenye nchi kama Bangladesh, Bolivia, Ecuador, Kyrgyzstan na Vietnam, na siku za hivi karibuni China na Urusi wamezizuia kutumika katika nchi hizo. Ili kusema mfumo huu ni halali au sio halali inategemeana na sheria za nchi husika.

Faida na hasara ya cryptocurrencies

bitcoin

Moja ya faida kubwa ya mfumo huu ni kutojulikana taarifa za mnunuaji au muuzaji. Japo taarifa za miamala kuwekwa wazi watu wote waone, hakuna taarifa binafsi zinazooneshwa kama jina au anwani ya muuzaji au mnunuaji

Cryptocurrencies ni maarufu kwa makundi ya kihalifu maana ni ngumu kujulikana

Ni faida na hasara kwa wakati mmoja. Cryptocurrencies ni maarufu kwa makundi ya kihalifu maana ni ngumu kujulikana. Hii ndio sababu kubwa serikali nyingi duniani zinazua matumizi ya Cryptocurrencies au zinajaribu kutengeneza mazingira ya uwazi wakati wa kununua au kuuza kwa kutumia mfumo huu.

Kutumia njia hii ya Cryptocurrencies kufanya biashara ni njia nzuri na rahisi japo kuna gharama ndogondogo ambazo unatakiwa ilipe kwa kila muamala unaofanyika ambao ni ndogo ukilinganisha na gharama zainazotozwa na mabenki.

Faida moja kubwa kuhusu Cryptocurrencies ni kuwa haiwezi kughushiwa, yani hakuna Cryptocurrency feki kama ambavyo hela za kawaida inavowezekana.

Usalama wa mfumo huu nao umekuwa ni moja ya changamoto kubwa. Kama tulivosema hapo mwanzo hizi hela zinahifadhiwa kwenye digital wallet ambapo mtu akifanikiwa kuhack anaweza kukuibia. na kwa wale wanaohifadhi kwenye kompyuta zao zilizo offline ikitokea hard disk ikafa au kuibiwa basi unakuwa umepoteza utajiri wako wote.

Changamoto iliyokubwa kuliko zote ni kwamba miamala inayofanyika kwa Cryptocurrencies uwa hairudishwi. Ikitokea unafanya biashara na mtu tapeli au kama hukuridhika na bidhaa uliyonunua basi hela yako inakuwa imeenda jumla. Tofauti na kutumia credit card hela yako inaweza kurudishwa iwapo haujaridhika na ulichokilipia na ukaamua kurudisha.

Cryptocurrencies kubwa unazotakiwa kuzijua

cryptocurrency

Bitcoin ndio kubwa kuliko zote na ndio maarufu zaidi duniani ikiwa na watumiaji mamilioni dunia nzima. Ilianzishwa na mtu au kikundi cha watu anaejiita Satoshi Nakamoto mwaka 2009. Kwa sasa kuna Cryptocurrencies tofauti tofauti zaidi ya 1000

Pamoja na kuwepo idadi kubwa, utagundua kwamba zinazotajwa sana ni zile kubwa kubwa zenye majina. Ambazo ni kama Ethereum (ETH) , Bitcoin Cash (BCH) , Ripple (XRP) , Dash (DASH), Litecoin (LTC) , Ethereum Classic (ETC)  na zingine nyingi. kwa mujibu wa taarifa kutoka CoinMarketCap.

Mijadala ya cryptocurrencies?

Tembelea link hizi hapa chini uweze kujisomea mambo mbalimbali kuhusu crypocurrencies.

  • CryptoCompare
  • Cryptocurrency Talk
  • Bitcoin Talk
  • Coingage
  • Bitcoin Wealth Club
  • BTC Warriors
  • Bitcoin Subreddit
  • Ethereum Subreddit
  • Litecoin Subreddit
  • Cryptocurrency Subreddit

Neno la mwisho

Tumeshaona sasa Cryptocurrency ni nini, inapatikanaje, inafanyaje kazi, hasara zake na faida zake. Mfumo huu wa manunuzi haushi leo japo sarafu ndogo ndogo zinaweza zikapotea ila kubwa kubwa kama bitcoin na Ethereum zitaendelea kuwepo kwa muda mrefu tu

Thamani ya Cryptocurrencies inaweza kupanda au kushuka kwa kiasi kikubwa cha dola kwa siku moja. Inashauriwa usitumie kiasi kibwa kuwekeza kwenye Cryptocurrencies ambacho hauko tayari kukipoteza

Ushawahi kutumia cryptocurrencies? Ipi? Tuandikie kwenye maoni yako.

KWENYE Bitcoin, Cryptocurrency
Sambaza chapisho hili
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Telegram Barua Pepe Nakili kiungo Durufu
Acha Ujumbe

Toa Jibu Ghairi kujibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Mtaawasaba Newsletter

Jiunge nasi kwa njia ya barua pepe tukujulishe kila inapotoka habari mpya

Zaidi Kutoka Mtaawasaba

Sasa unaweza pata Blue Tick kwa kulipia Instagram na Facebook

Sasa unaweza pata Blue Tick kwa kulipia Instagram na Facebook

Siku 4 zilizopita
Airtel yawa ya kwanza kuzindua huduma ya kadi za eSIM Tanzania

Airtel yawa ya kwanza kuzindua huduma ya kadi za eSIM Tanzania

Siku 5 zilizopita
Instagram yazindua Notes, Candid Stories, na Zaidi

Instagram yazindua Notes, Candid Stories, na Zaidi

Miezi 3 iliyopita
Umoja wa Ulaya waishinikiza Apple kuruhusu maduka mbadala ya programu kwenye iPhones na iPads

Umoja wa Ulaya waishinikiza Apple kuruhusu maduka mbadala ya programu kwenye iPhones na iPads

Miezi 3 iliyopita

© 2013 - 2023 Mtaawasaba Interactive. Crafted by Simba Creative

  • Kuhusu Sisi
  • Sera ya faragha
  • Vigezo na Masharti
  • Wasiliana Nasi
Go to mobile version
logo logo
Karibu Mtaawasaba!

Jaza taarifa kuingia Kwenye Akaunti Yako

Umesahau Nywila?