Elon Musk ametangaza rasmi vita na Apple

Mwandishi Amos Michael

Mtu tajiri zaidi duniani na mmiliki wa Twitter, Bilionea Elon Musk ametangaza rasmi vita na Apple, kampuni kubwa zaidi ya teknolojia duniani.

Elon Musk ameishutumu Apple katika tweets zake nyingi za hivi karibuni kuhusu mazoea ya ukiritimba na udhibiti. Musk alidai kuwa kampuni hiyo ilisitisha matangazo kwenye mtandao wa Twitter na kuhoji ikiwa Apple na Mkurugenzi Mtendaji wake Tim Cook wanachukia uhuru wa kujieleza nchini Marekani.

Apple pia imetishia kuzuia Twitter kutoka kwa duka lake la App, lakini haitatuambia sababu. – Elon Musk

Musk alituma ujumbe Twitter akitoa sababu ya ukosoaji wake wa hivi karibuni. Hata hivyo, Apple hawajajajibu hata mara moja kwenye tweet yoyote ya Musk.

Zaidi ya hayo, Musk pia alidai kuwa ada ya 30% ambayo Apple huchukua kutoka kwa mauzo mengi kupitia duka la App la kampuni hiyo. Katika tweet iliandikwa, “lipa 3% au nenda vitani” na gari kuchagua njia ya gobtobwar.

Pia Musk amekosoa kodi ya 30% inayotozwa na duka la programu la Apple kuwa ni kubwa kupita kiasi. Sio Musk peke yake ambaye amelalamikia hili kwani, kuna mzozo wa kisheria unaoendelea kati ya msanidi programu wa mchezo wa video wa ‘Fornite’ Epic Games.

Hii sio mara ya kwanza Musk kukosoa duka la programu ya Apple hapo awali, mnamo Mei Musk alisema ada ya 30% ilikuwa “mara 10 zaidi kuliko inavyopaswa kuwa”.

Miongozo inayutuiwa kwenye duka la programu la Apple inayolalamikiwa na Musk ilipelekea kufungiwa kwa program za Discord, Tumblr na zingine zenye maudhui ya kutatanisha (hasa ya kikubwa) mpaka hapo zitalipoondoa maudhui yenye utata. Hata hivyo Twitter inaendelea kuwa na maudhui ya kikubwa, na hii inaweza kuwa sababu mojawapo ya kuondolewa kwa programu ya Twitter.

Katika miongozo yake rasmi ya ukaguzi wa duka la programu, Apple inaorodhesha vigezo mbalimbali vya usalama ambavyo programu lazima zizingatie ili zijumuishwe dukani, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuzuia “maudhui ambayo ni ya kukera, yasiyofaa, ya kukasirisha, yaliyokusudiwa kuchukiza, pia itatakiwa kuzuia mamb kama vile matamshi ya chuki, picha za ngono na ugaidi. “Ikiwa unatafuta kuwashtua na kuwaudhi watu, Duka la App sio mahali sahihi kwa programu yako,” miongozo hiyo inasema.

Avatar of amos michael
Mwandishi Amos Michael Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
Meezy ni mchangiaji wa machapisho mbalimbali hapa Mtaawasaba tangu kuanzishwa kwake. Meezy ni mpenzi wa Android na anapokuwa nyumbani hupendelea kupiga kinanda na kuandaa muziki
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive