Elon Musk anunua asilimia 9.2 ya hisa za Twitter, na kuwa mdau mkubwa

Mwandishi Emmanuel Tadayo
Kwa mujibu wa taarifa kutoka soko la hisa huko Marekani zinasema, Elon Musk anunua asilimia 9.2 ya hisa za Twitter ambazo ni sawa na dola za kimarekani billioni 2.89 kwa mujibu wa viwango vya soko siku ya ijumaa, na kumfanya kuwa ndiyo mmiliki mkubwa wa hisa za kampuni hiyo.

Hisa za mtandao wa kijamii wa Twitter zilipanda ghafla kwa asilimia 27 kufuatia taarifa ya Elon Musk kununua hisa. Upandaji huu mkubwa wa hisa za kampuni hii haujawahi tokea mwaka 2013 Twitter walianza rasmi kuruhusu watu kununua hisa za kampuni hiyo.

Elon Musk mwenyewe hajasema sababu zilizomsukuma kununua hisa hizo au mipango yake kwenye kampuni hii. Hata hivyo amekuwa mkosoaji mkubwa wa sera za mtandao wa Twitter hasa kuhusu uhuru wa kujieleza. Mwezi uliopita alisema ana “mpango serious” wa kuanzisha mtandao wake wa kijamii. 

Elon Musk hatajiunga na bodi ya wakurugenzi Twitter

Elon Musk hatajiunga na bodi ya wakurugezi wa Twitter, hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na mkurugenzi mtendaji wa Twitter bwana Parag Agrawal ambaye aliandika kupitia mtandao huo wa kijamii. Elon alitarajiwa kukaribishwa kwenye bodi ya wakurugenzi siku ya jumamosi akiwa kama mmiliki mkubwa wa hisa ila siku hiyo hiyo alighairi na mpaka sasa haijasemwa ni kwa nini ameghairi kujiunga

Avatar of emmanuel tadayo
Mwandishi Emmanuel Tadayo Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
mwandishi wa habari za teknolojia kwenye tovuti pendwa ya mtaawasaba
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive