Fahamu kuhusu Gari ya Umeme

Mwandishi Diana Benedict

Gari la umeme ni gari ambalo linatengenezwa na motor moja au zaidi ya umeme, kwa kutumia nishati zilizohifadhiwa kwenye betri za kuchaji. Magari ya kwanza ya umeme yalizalishwa katika miaka ya 1880. Magari ya umeme yapata umaarufu mwishoni mwa karne ya 19 na mapema karne ya 20, Mwaka 1897 magari ya umeme ndio yalianza kutumiwa kibiashara huko Marekani. Wazalishaji wa magari ya umeme wanaosifika sana kati yao ni Tesla, BMW, Range Rover na makampuni mengine mengi.

Range Rover PHEV 400e

 

Magari ya umeme ni Magari ambayo hufanya uchafuzi wa hali ya chini katika mazingira yanayotuzunguka kuliko magari yanayotumia petroli au diesel, hivyo magari haya ni mazuri kwa mazingira kuliko magari ya petroli (hasa katika miji).

Uhifadhi wa Umeme

Magari haya  ni magari yanayotumiwa na seli na motor ya umeme kushinda magari ya Petroli yanayotumia injini. Magari ya Petroli hutumia injini ambayo inasukumwa na piston kwahiyo huhitaji kutunza mafuta kwa ajili ya kwenda umbali mrefu, Tofauti na magari haya ya umeme yenyewe hutunza umeme kwenye seli (Chipsi zilizoungana) za umeme.

Kucharg gari kunaweza kuchukua muda wa hadi saa, hata hivyo kiasi hiki cha muda kinazidi kupungua kadri teknolojia inavyo endelea kuboreshwa. Kwa sasa kuna miundombinu isiyofaa ya katika magari haya hasa katika kurejea kucharg, ingawa wamiliki wengi hutumia vituo vya nyumbani badala ya miundombinu ya biashara. Vipimo vya gharama za betri na huongezeka kutokana na ukubwa gari unayohitaji.

car batter

Spidi Na Ubadirishaji Gear

Magari ya Umeme ni Magari yasiyo na injini ya kawaida, Yanatumia motor za umeme ambazo, Pia magari haya yanakuja na automatic transmision amabyo yanaweza kutoka speed ya 0 – 100KM kwa muda usiozidi sekunde 30.

06 i8 Workshops

 

Magari haya ya umeme bado hayatazamiwa kutumika Tanzania, kwa sasa yanatumika marekani na nachi zilizoendelea kiteknolojia.

Endelea kutufuatilia kwenye mitandao mbali mbali ili usipitwe na Habari, Uchambuzi naMakala mbali mbali ya mitanadoni na ya kiteknolojia kwenye FacebookTwitterInstagram, Google+ na Youtube, Pia usisite kutoa maoni yako hapo chini au tuandikie barua pepe kwa mhariri@mtaawasaba.com

Mwandishi Diana Benedict Mwandishi
Mitandao ya Kijamii
Diana Benedict. Digital Creator | IT Specialist | Graphics Designer | Web Designer | Web SEO | Contents Management | UI/UX Designer and Social Media Management.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive