FMWhatsApp yatumika kusambaza virusi

Mwandishi Alexander Nkwabi

Imegundulika app ya FMWhatsApp yatumika kusambaza virusi vyenye uwezo wa kusoma SMS kwenye simu ya mtumiaji.  Kampuni ya ulinzi mtandaoni ya Kaspersky imegundua kirusi kwenye toleo lisilo rasmi la WhatsApp (lililochakachuliwa) maarufu kwa jina la FMWhatsApp. Kirusi hiki kwa jina Triada mobile Trojan, hu download virusi wengine kwenye simu ambapo huweza kufungua matangazo na kusoma SMS za mwenye simu husika.

WhatsApp ni moja ya apps maarufu kwa kutuma na kupokea messages, japo kuwa baadhi ya watu hutaka features zaidi kama vile kuweza kusoma status au kuona picha zilizofutwa, hivyo kushawishika kutumia WhatsApp iliyochakachuliwa kwa sababu huzikosa kwenye ile yenyewe.

Wanaochakachua apps hizi hujaribu kuweka matangazo ili kujiingizia kipato, ambapo kwa upande mwingine huwapa fursa matapeli kutumia fursa hii kuingiza virusi kupiti matangazo.

Kwa mfano FMWhatsapp toleo 16.80.0 limeonekana na kirusi aina ya Triada Trojan kwenye code zake. Ambacho kinatumika kama mlango wa kuruhusu virusi wengine kuingia kwenye simu husika.

FMWhatsApp yatumika kusambaza virusi

Kirusi hiki kilicho kwenye FMWhatsApp kinafanya nini:

  1. Kwanza, hukusanya taarifa za kifaa cha mtumiaji kisha,
  2. Hudownload kirusi kingine kwenye simu ya mtumiaji.
  3. Virusi vinaweza kufungua na kuonesha matangazo kwenye simu vyenyewe,
  4. Pia, vitamuunga mtumiaji kwenye huduma za kulipia
  5. Mwisho vina uwezo wa kusoma sms zenye namba ya uthibisho kwenye simu ya mtumiaji, hivyo kumuweka kwenye hatari.

“App hizi zilizochakachuliwa sio nzuri kwa matumizi lakini sio rahisi kwa watumiaji kuziacha kwa sababu zina vitu vile wanavyovihitaji, hii huwaweka katika hatari ya kukumbwa na wahalifu wa mitandaoni. Nashauri watumiaji wajikite katika kutumia apps zinazotoka kwenye app store zinazoeleweka hata kama hazina makorokoro mengi,” alisema bwana Igor Golovin, ambaye ni mtaalam wa maswala ya ulinzi kwenye kampuni ya Kaspersky

 

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive