Google kutengeneza Miwani Janja (Smartglasses)

Mwandishi kasomi
Kampuni ya Google kutengeneza Miwani Janja (Smartglasses) mpya. Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinadai Kampuni ya Google iko mbioni kuingia katika soko la Miwani janja za AR na imeanza majaribio ya kutengeneza AR Glasses zake.

Mpaka sasa kampuni za simu na mitandao ya kijamii za Snapchat, Ray Ban, Meta, TikTok, Xiaomi, Oppo na Huawei zimeshatoa miwanijanja zao mpya ambazo zina uwezo wa Augmented Reality. Na pia kampuni ya Apple pia ipo katika matengenezo na inaunda Smart Glasses zake.

Mwaka juzi Google iliinunua kampuni ya North ambayo inayohusika na kutengeneza smart glasses za Focals 2.0. Google inajipanga kujaribu kutengeneza smart-glasses zake na ipo katika mchakato wa kutengeneza na inategemewa itatoka mwaka huu.

Faida kubwa ya miwani janja za Google ni kuwa zinakuja na Google Lens, Google Assistant na mfumo mzuri wa AR hivyo itakuwa ni miwani janja na yenye akili kwa kuunganisha na mfumo wa Google.

Itakuwa ni maalum kwa wanafunzi, designers, madaktari na wataalam mbalimbali. Tofauti na VR kama za Sony na Meta; AR (Augmented Reality) glasses ni simple na inatumia mazingira yaliyopo kuongeza details za ziada kama vile infos, notifications, directions na mtu anaona mbele kama kawaida huku akiwa anaona details za ziada.

Kwa sasa kampuni kubwa za Tech zinajikita kwenye soko la miwani janja za AR baada ya Snapchat, Ray Ban na Facebook kufanikiwa katika AR Glasses.

Mwandishi kasomi Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
Mwandishi | mhamasishaji | mwanafalsafa | blogger | Host | Personalty TV & Radio presenter @Kasomi TV
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive