Facebook na Ray-Ban waja na miwani janja yenye uwezo wa kupiga simu, picha na zaidi

Mwandishi Alexander Nkwabi
Ni takribani miaka saba sasa tangu kampuni ya Google ilipokuja na bidhaa yake ya Google Glass iliyoshindwa kabisa kuteka soko la wapenzi wa teknolojia mpya, na miaka mitano iliyopita Snapchat walikuja na Spectacles, miwani janja ambayo haikuteka soko pia lakini bado ipo sokoni. Leo Facebook na Ray-Ban waja na miwani janja yenye uwezo wa kupiga na kupokea simu, picha, kurekodi video, kucheza podcast na zaidi.

Miwani janja hii iliyopewa jina la Ray-Ban Stories, tayari imeingia sokoni na kwa sasa inapatika katika nchi za Marekani, Australia, Canada, Ireland, Italy, na Uingereza. Miwani hii unaweza kuipata kwa dola za kimarekani 299 sawa na shilingi za kitanzania laki saba. Na inakuja kwa zaidi ya mionekano ishirini.

Facebook na Ray-Ban waja na miwani janja

Katika chapisho kutoka kwenye blogu ya Facebook, wameandika miwani hii itawawezesha watu kurekodi matukio moja kwa moja yanapotokea katika mtazamo wa kipekee kabisa, pia utaweza sikiliza muziki, kuongea na watu kutumia app ya Facebook View, kusambaza picha na video kwenye mitandao ya kijamii.

Unapoiona miwani hii kwa mara ya kwanza waweza dhani ni ya miwani ya kawaida tu ya Ray-Ban ila kwa ndani miwani hii ina kamera mbili zenye 5MP, pia miwani hii ina bluetooth 5.0, na wi-fi ambayo ina jiunga na simu yako, betri, nafasi ya kuhifadhi picha mpaka 500 na spika.  Unaweza kupiga picha kwa kubonyeza kitufe upande wa kulia wa miwani.

Miwani hii haifanyi kazi yenyewe kama yenyewe ila inahitaji uwe na simu ya iPhone au Android na iwe na app ya Facebook View, pia itahitaji kuungasha bluetooth na Wi-Fi kwenye simu hiyo ili iweze kutumia huduma za kupokea na kupiga simu kusambaza picha.

 

Facebook View app
Facebook View app

Watu wengi uwa na wasiwasi kuhusu faragha, Facebook wamesema mtumiaji ataweza kuzipata taarifa zake zote na kuzifuta muda wowote anaotaka, pia anaweza kuzuia uwezo wa miwani hizo kurekodi sauti. Facebook wamesisitiza kuwa picha na video kwenye miwani zitakuwa encrypted ili kuongeza ulinzi.

Mwisho, Facebook wanasema ni akaunti moja tu itatumika na miwani kwa wakati mmoja, na ikitokea miwani kupotea au mtu kutaka kubadili akaunti basi taarifa zote za awali zitafuta moja kwa moja.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive