Google waja na app ya kukusaidia kudhibiti matumizi ya data

Mwandishi Alexander Nkwabi

Vifurushi vya data ni bei ghali sio nchini kwetu bali nchi nyingi duniani. Unapokuwa unatumia simu yako kuchat, kufungua mitandao ya kijamii au kuangalia video Youtube pia unakuwa unaangalia usitumie data kwa kiasi kikubwa. Na ni ngumu kujua ni app gani inatumia sana data kuliko zingine.

Datally inamsaidia mtumiaji kuelewamatumizi ya data kwa kutoa ripoti ya kila saa, siku , wiki na mwezi. Pia inamshauri mtumiaji njia za kubadili matumizi ili kuokoa data.

qmfkih5jpx4kytnynoqt

Datally ina data saver, inayoweza kuzuia ulaji wa data hata kama app haitumiki na inafatilia matumizi ya kila app kwenye simu ya mtumiaji. Kamainatokea app moja inakula sana data kuliko kawaida, mtumiaji anaweza kuizima app iyo bila kuathiri matumizi ya app zingine.

Mwisho, Daally inaweza kumsaidia mtumiaji kuhifadhi data kwa kumtaarifu pindi anapokuwa karibu na eneo lenye mtandao wa WI-FI wa wazi.

Google wameifanyia majaribio Datally kwa miezi kadhaa huko nchini Ufilipino na imeonekana watu wameweza kuhifadhi data mpaka asilimia 30, kabla ya kuiachia kwa dunia nzima hivi leo. Unaweza kuijaribu Datally kama unatumia simu ya Android kuanzia Lollipop5.0 na inapatikana Google Play.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive