Sasa Programu ya ChatGPT kupatikana na watumiaji wa Android

Amos Michael Maoni 2

OpenAI kampuni nyuma ya programu saidizi ya akili bandia imetangaza kuwa itatoa programu ya ChatGPT kwa watumiaji Android. Programu hiyo itaanza kupatikana kuanzia wiki ijayo na inapatikana kwa ku pre order kwenye Duka la Google Play.

Habari hii inakuja baada ya programu rasmi kwa watumiaji wa iOS kutolewa mwezi Mei na kampuni hiyo ikisema toleo la Android litaanza kupatikana hivi karibuni. Programu hii ni bure na itasawazisha historia ya matumizi yako kwenye vifaa vyote.

ChatGPT ilipata umaarufu mkubwa kwa muda mfupi baada ya uzinduzi wake mnamo Novemba mwaka jana, na kupata watumiaji milioni 100 ndani ya miezi miwili tu baada ya uzinduzi wake.

Programu hii inatoa msaada mkubwa kwa watumiaji wake kwa kufanya mazungumzo mafupi, kuandika insha, muhtasari, kuandika upya maandishi marefu kwa namna tofauti na kadhalika. Programu hii sasa itapatikana kwenye kivinjari cha edge.

Kwa mujibu wa mtandao wa similarweb, matumizi ya programu hii yameshuka kwa asilimia 9.7 kwa watumiaji wa mtandaoni na pia idadi ya watumiaji wapya imeshuka. Kuanza kupatikana kwenye mfumo endeshi wa Android kutasaidia kuongeza idadi ya watumiaji wapya.

Kumekuwepo na malalamiko kwa baadhi ya watumiaji wa #ChatGPT kuwa imepunguza kasi na ufanisi, na hata baadhi yao kuhisi OpenAI wamefanya makusudi ili kupunguza kasi ya watumiaji kuitegemea kwa kiasi kikubwa, madai ambayo OpenAI wameyakanusha.

MADA:
Mwandishi Amos Michael Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
Meezy ni mchangiaji wa machapisho mbalimbali hapa Mtaawasaba tangu kuanzishwa kwake. Meezy ni mpenzi wa Android na anapokuwa nyumbani hupendelea kupiga kinanda na kuandaa muziki
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive