Jinsi Fingerprint sensor inavyofanya kazi juu ya kioo cha simu

Diana Benedict 1
Kipindi kirefu kimepita tangu uvumi wa Sensa ya kidole kuwekwa juu ya kioo cha simu cha kuonesha, Tumezoea kuona ulinzi wa sensa ya kidole (Fingerprint) kuwekwa chini mwisho wa mipaka ya kioo au nyuma ya simu, Kampuni kama Apple na Samsung zilitarajiwa kuifanya teknolojia hii kabla ya kufikiri makampuni mengine, Lakini mwanzoni mwa mwaka huu kampuni ya VIVO imefanikiwa katika hilo na kuweza kuzindua Simu yao mpya iliyowekwa Sensa ya kidole juu ya kioo cha simu cha kuonesha. Chapisho hili litakuelezea kwa kina Jinsi Fingerprint sensor inavyofanya kazi.

 

vivo inbuilt fingerprint sensor 1

Kwa hali ya kawaida ni ngumu kuamini kuwa unaweza kuweka ulinzi wa kidole juu ya kioo cha simu yako lakini hapa utapata majibu ya swali lako kuhusu Sensa hiyo.

Kwanza kabisa kabla ya yote Ungependa kujua Sensa ya kidole (Fingerprint) ni nini?

Sensor ya kidole ni kifaa cha umeme kinachotumiwa kukamata picha ya digital ya muundo wa vidole. Picha iliyokuwa captured inaitwa live scan. Scan hii inafanya mchakato ili kuunda template ya biometri (mkusanyiko wa vipengee vilivyotengwa kwenye kidole) ambavyo vinahifadhiwa na kutumika kwa kulinganisha data hizo. Teknolojia nyingi zimetumika ikiwa ni pamoja na macho (Iris Scarner au FaceID), Vifaa vingi vimekuwa vikitumia mfumo huu wa Sensa ya kidole kama mfumo wa ulinzi kwenye simu yako na imekuwa ikisaidia sana hasa katika jamii yetu ya Tanzania.

Simu nyingi zinazoundwa miaka hii zimekuwa ni simu za kuweka karibia asilimia 99 ya kioo kuonekana na kupelekea baadhi ya vitu kufikiria pa kuviweka ikiwa bado vina umuhimu katika ufanyaji kazi wa simu, hasa katika uli, makampuni mengine kama Google Pixel, Samsung S8, S8 plus, Huawei, Tecno wao waliona kuhamishia Sensa ya kidole nyma ya simu, lakini bado imekuwa ni Tatizo kwa wwatu wengine hata katika kupeleka kidole nyuma ya simu.

vivo fingerprint phone and chip cs

 

Jinsi Sensa Inavyofanya Kazi

Simu ya kwanza kuwekwa Sensa ya kidole juu ya kioo cha kuonesha ni VIVO, Sensa hii imewekwa ndani ya kioo cha simu upande wa chini, ambayo inapitisha mionzi yake juu ya kioo na kuweza kutambua alama za vidole. Katika hardware sensa hiyo iko chini ya kioo ambayo unaweza ukaiona kama utaweza kuitazama kwa makini, Ni sensa ambayo ni transparent iliyowezeshwa kukaa juu ya kioo na kutambua vipengele vya kidole kama zilivyo sensa za kawaida. Tofauti niliyoipata katika simu hii ni kwamba bado haijaweza kufuta historia ya sensa za kawaida kwakuwa bado inafanya kazi taratibum unaweza tumia kama sekunde 1.5 kufungua simu ukilinganisha na sensa za kawaida mabazo zinafungua simu chini ya sekunde moja.

Natumai Somo hili limekunufaisha kwa namna moja ama nyingine, Endelea kuwa nasi kwa kutufuata kwenye mitandao ya kijamii, na usisahau ku subscribe ili uwe wa kwanza kupata Habari, Uchambuzi na Makala mbali mbali za kisayansi na teknolojia. Pia usisahau ku acha maoni yako hapo chini na unaweza kuwasiliana nasi kwa barua pepe [email protected]

Mwandishi Diana Benedict Mwandishi
Mitandao ya Kijamii
Diana Benedict. Digital Creator | IT Specialist | Graphics Designer | Web Designer | Web SEO | Contents Management | UI/UX Designer and Social Media Management.
1