Kampuni ya Nokia kuungana na Vodacom Kueneza teknolojia mpya ya 5G

Mwandishi Diana Benedict

Nokia na Vodacom wametangaza ushirikiano kati ya makampuni haya mawili kushirikiana katika majaribio ya mtandao kuanza kutumia teknolojia ya Nokia 5G ambayo pia itawawezesha Vodacom kuendeleza digitali kwa manufaa ya biashara na watu binafsi Africa.

61546156

Nokia itashiriki uvumbuzi wake wa hivi karibuni wa 5G ikiwa ni pamoja na kuzindua Antennas nyingi za kupitisha MIMO, AirScale Radio Access, AirGile Cloud-native Core, Multi-Access Edge Computing, na end-to-end Mobile Anyhaul transport networks ili kuchunguza jinsi ya kuweza kutumiwa kulingana na mahitaji yanayohitajika.

Makampuni yatazingatia utoaji wa huduma za video za kweli za Ultra-HD na virtual, kwa kutumia kiwango kikubwa cha mobile broadband na ultra-low latency capabilities za 5G. Vodacom na Nokia pia watashirikiana kutambua jinsi gani 5G itaweza kuendesha ukuaji wa uchumi katika viwanda muhimu kwa ikiwa ni pamoja na viwanda vya madini, huduma za afya, vyombo vya habari, nishati na usafiri.

Vodacom logo

Andries Delport, Afisa Mkuu wa kitengo cha Teknolojia ya Vodacom alisema hivi: “Kama mtoa huduma wa mtandao wa simu za mkononi Afrika, na mitandao bora ya 3G na 4G, ilikuwa muhimu kwa sisi kushirikiana na kampuni yenye kuvutia kama Nokia kama tunavyojishughulisha kwenye kizazi kijacho cha mitandao. Ushirikiano huu unakuja wakati ambapo tuna mamlaka imara kutoka kwa Bodi ya Vodacom kuhamasisha Vodacom Group kuwa kampuni inayoongoza ya digitali. Ni imani yangu imara kuwa kupitishwa kwa 5G kutatusaidia kutoa baadhi ya teknolojia za digital katika maeneo kama vile uchambuzi mkubwa wa takwimu, ukweli halisi na uliodhabitiwa, autonomous vehicles na Mambo ya internet. Kwa kifupi kabisa, Afrika teknolojia ya 5G itatusaidia kutoa kasi ya mtandao kwa wateja wetu karibu milioni 70 katika”.

Tufuatilie @MtaawaSaba ili usipitwe na Habari, Uchambuzi naMakala mbali mbali ya mitanadoni na ya kiteknolojia kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Google+ na Youtube, Pia usisite kutoa maoni yako hapo chini au tuandikie barua pepe kwa mhariri@mtaawasaba.com

Mwandishi Diana Benedict Mwandishi
Mitandao ya Kijamii
Diana Benedict. Digital Creator | IT Specialist | Graphics Designer | Web Designer | Web SEO | Contents Management | UI/UX Designer and Social Media Management.
1 Comment

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive