Kampuni za simu kuboresha usajili wa wateja kwa kutumia alama za vidole

Mwandishi Alexander Nkwabi

Leo karibu mitandao yote ya simu nchini Tanzania imekuwa ikituma ujumbe mfupi wa maneno kwa wateja wao unaosema “Ndugu mteja katika kuboresha usajili wa laini za simu alama za vidole zitatumika kuanzia Februari 5, 2018. Kwa mawasiliano zaidi tembelea maduka yetu,”

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema kampuni za simu za mikononi zitaanza upya kusajili laini za wateja wao kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kielektroniki inayohusisha uchukuaji wa alama za vidole.

pictcra

Akitoa ufafanuzi, Bwana Semu Mwakyanjala ambaye ni Kaimu meneja mawasiliano kwa umma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) alipoulizwa na mwandishi wa gazeti la Mwananchi kuuliza kuhusu ujumbe unaotumwa kwa wateja kutoka kampuni za simu za mkononi ukiwajulisha kuhusu usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole. alisema

mfumo huo unaotumia alama za vidole na picha ni wenye uhakika ambao ni vigumu kughushi. Walishafanya majaribio kuhusu mfumo huo na kuona unafaa.

“Huu ni usajili wa kielektroniki ambao unaiwezesha kampuni na mamlaka kupata taarifa mbalimbali za mteja kwa muda mfupi,” alisema.

Akifafanua zaidi alisema, TCRA imeziruhusu kampuni zote za simu za mkononi kutumia mfumo huo.

Kampuni ya Airtel itakuwa ya kwanza kuutumia mfumo huo mpya kwa majaribio, aliyasema hayo bwana Jackson Mmbando ambae ni meneja uhusiano wa Airtel Tanzania, anaamini mfumo huu wa kusajili laini za wateja kwa njia ya vidole ni njia salama zaidi.

Mikoa ambayo Airtel itaanza nayo kwa mpango huo wa majaribio utahusisha mikoa minne ambayo ni Dar es Salaam, Pwani, Iringa na Singida. Pia, utafanyika Zanzibar. Ambapo wataanza kwa kusajili wateja wapya kwa kutumia alama za vidole. Ambapo baadaye wataendelea kwa wateja wengine hata ambao walishasajili laini kupitia mfumo wa zamani.

Endelea kutembelea tovuti ya Mtaawasaba ili uweje kujua zaidi ya Airtel ni mitandao ya simu ipi itafuata kwenye utaratibu huu mpya wa kusajili line mpya kwa kutumia alama za vidole.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive