Kutoka MWC 2018: HMD Global yazindua simu nne za Nokia kwa mpigo

Mwandishi Alexander Nkwabi

HMD Global kampuni inayotengeneza simu za Nokia leo imezindua simu nne kwa mpigo ikiwemo Flagship yake ya kwanza tangu waanze kutengeneza simu zenye nembo ya Nokia na simu ingine ambayo ni moja ya simu za mwanzo kabisa kutumia toleo la Android One hasa toleo la Go. Haya yamejiri katika onesho waliloandaa kwa ajili ya uzinduzi wa simu hizi kwenye kongamano la MWC 2018.

Nokia 1

nokia 1Simu hii inatarajiwa kuuzwa kwa dola za kimarekani 85 ambazo ni takribani shilingi laki 2 za kitanzania. Itaanza kuuzwa kuanzia mwezi wa nne 2018. Simu hii inakuja na rangi mbili Nyekundu na bluu iliyokoza. Nokia 1, ambayo ni simu ya bajeti ndogo inayotumia Android Oreo Go Edition. Baadhi ya sifa za simu hii ni kioo chenye upana wa inchi 4.5, Kamera yenye 5-megapixel na LED flash, pia ina kamera ya selfie yenye 2-megapixel, sifa zingine ni mfumo endeshi ni inatumia ni Android Oreo Go. Simu hii inakuja naBetri inayotoka yenye 2,150 mAh. Sifa zaidi soma kwenye uchambuzi wa simu hii. Simu hii itakuwa optimized kutumia Go apps ambazo baadhi ni app za google ikiwemo YouTube, Gmail, Gboard, Assistant na zingine nyingi.

Nokia 6 (2018)

Jina halisi la simu hii ni Nokia 6 (second generation) na inaonesha itakuwa na karibu sifa nyingi za mtangulizi wake aliyetoka mwaka jana Nokia 6 (2017). Simu hii inakuja na mfumo endeshi Android Nougat ambapo inaweza kupandishwa hadhi mpaka Android Oreo.

Simu hii inakuja na chip ya Qualcomm Snapdragon 630 (mtangulizi wake alikuja na Snapdragon 430) pia inakuja na teknolojia ya kurekodi sauti ya OZO, na itakuwa na Bothie photo mode kwenye upande wa kamera. Uchambuzi wa simu hii usome hapa

Nokia 7 Plus

1518677033 nokia7plus story

Simu hii ni kaka mkubwa wa Nokia 6 hii toleo jipya maana zinafanana kwa ujumla. Simu hii inakuja na kioo kikubwa chenye upana wa inchi 6 na resolution ya 2220×1080 ambayo ni sawa na uwiano wa 18:9. Kamera zilizoboreshwa kabisa zenye 12-megapixel wide aperture sensor na 13-megapixel telephoto kwa upande wa nyuma, pia kamera yenye 16-megapixel kwa mbele. Simu hizi zina nembo maarufu ya Zeiss

 

 

Nokia 8 Sirocco

Nokia 8 Sirocco CameraKulikuwa na tetesi za Nokia 9 kuzinduliwa China mwaka huu mwanzoni, ila kumbe ilikuwa ni Nokia 8 Sirocco. Simu hii ambayo ndiyo simu yenye sifa kubwa kuliko zote ambazo mpaka sasa zimetengenezwa chini ya HMD Global inakuja na prosesa ya Snapdragon 835, RAM 6GB na ina nafasi ya 128GB na itakuwa na mfumo endeshi wa Android One. Simu hii ambayo itaanza kupatikana nchi za ulaya kuanzia mwezi wa nne mwaka huu inatarajiwa kuuzwa kiasi cha euro 749.

Uchambuzi zaidi kuhusu smu hii unakuja muda si mrefu.

 

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive