Kwa heri iPod. Apple yasitisha rasmi uzalishaji wa iPod

Mwandishi Alexander Nkwabi
Baada ya karibu miaka 21, iPod hatimaye imefikia mwisho wake. iPod ya kwanza kabisa ilitolewa Oktoba 23, 2001 na sasa Apple imetangaza rasmi kusitisha uzalishaji wa music player hii ya kipekee iliyoleta mapinduzi makubwa katika uwanja wa muziki. iPod ya mwisho kuingia sokoni ni iPod Touch ya kizazi cha 7.

Apple ilitangaza habari hii kupitia chapisho rasmi la blogu , ikisisitiza kwamba hakuna kitu cha kusikitisha. Kampuni ikaendelea kusema kwamba imeunganisha kwa usalama uwezo wa iPod katika bidhaa nyingine za Apple , kuanzia iPhone hadi HomePod mini. Kwa hivyo, inawashawishi watu kutazama machaguo haya kwa sasa.

Hii ni dalili nyingine ya ukweli kwamba huenda hatuhitaji bidhaa maalum ili kusikiliza muziki, kwa kuzingatia kwamba iPhone au hata simu ya Android inathibitisha kuwa inatosha. Na hapa ndipo iPod ” inaishi! ”

Makamu wa Rais Mkuu wa Apple wa Masoko, Greg Joswiak, alisema, ” Leo, iPod inaendelea kuishi. Tumeunganisha hali nzuri ya muziki katika bidhaa zetu zote, kuanzia iPhone hadi Apple Watch hadi HomePod mini, na kwenye Mac, iPad na Apple TV. Na Apple Music hutoa ubora wa sauti unaoongoza katika tasnia kwa usaidizi wa sauti za anga – hakuna njia bora ya kufurahia, na kugundua muziki. ”

iPod touch, ambayo iliachiwa mwaka wa 2019, ndiyo ilikuwa ya mwisho katika bidhaa ya iPod. IPod ya kwanza ilianzishwa mnamo Oktoba 23, 2001, karibu miaka 21 iliyopita . Baada ya hapo kulikuwa na uzinduzi wa iPod mini mnamo 2004, nano (2nd Gen) mnamo 2006, iPod Touch ya kwanza mnamo 2007, nano (7th Gen) mnamo 2012, shuffle (4th Gen) mnamo 2015, na hatimaye iPod touch ndiyo ya mwisho sasa.

Lakini, hii sio habari mbaya kabisa. Apple bado inauza iPod touch kupitia maduka yake na wauzaji walioidhinishwa hadi hifadhi itakapomalizika. Inauzwa kwa dola za marekani 199 kwa muundo wa 32GB , dola 299 kwa muundo wa 128GB, na dola 399 kwa muundo wa 256GB. Kwa hivyo, ikiwa unataka kupata uzoefu wa iPod kwa mara ya mwisho au hatimaye kutimiza ndoto ya kumiliki moja kwa ajili ya nostalgia, unaweza kufanya ununuzi.

Una maoni gani kuhusu hatua hii? Je, unadhani Apple ilipaswa kuendelea kutengeneza? Tujulishe mawazo yako katika maoni hapa chini.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive