Katika tangazo kwa umma lililo chapishwa kwenye akaunti ya Twitter ya Shirika la simu Tanzania (TTCL) linasema kuwa wananchi waepuke matapeli wanao uza line za simu za mtandao huo, taarifa hiyo imeongeza kuwa line za simu zinatolewa bure kupitia maduka yao, vituo vya huduma kwa wateja na kwenye miamvuli ya TTCL ambayo hupatikana maeneo mbali mbali ya wazi nchini.
Unachotakiwa kufanya tu nikununua salio la muda wa maongezi kuanzia shilingi mia tano na kuendelea ili ku activate line yako.
TTCL ambayo kwa sasa inaongeza kasi katika maboresho ya huduma zake ili kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma bora za mawasiliano kwa gharama nafuu. Baadhi ya huduma zinazotolewa na TTCL ni pamoja na vifurushi vya kupiga simu, pamoja na data kwa gharama nafuu kabisa labda kuliko mtandao wowote kwa sasa. Na kwa sasa wana mradi wa kusambaza intaneti majumbani wakianzia mkoani dar es salaam na dodoma kisha mradi huo utasambaa nchi nzima,
Laini za simu za TTCL zinatolewa bure
Mwandishi
Alexander Nkwabi
Mhariri
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta.
Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako
Maoni yako